Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai akiangalia shughuli za uzalishaji zilizofanywa na vijana walionufaika na mradi wa Kijana Jitambue yaliyohitimishwa Mkoani Tabora akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Miradi Care International Tanzania na Mratibu wa FEMA Tanzania.
Na Mwandishi Wetu.
Vijana wa Shule za Sekondari kutoka Mikoa ya Shinyanga na
Tabora wametakiwa kujiepusha na vitendo viovu vinavyosababisha wao kushindwa kutimiza ndoto zao.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai wakati akifunga mafunzo kwa vijana wa kike na kiume kutoka Shule za Sekondari kutoka Mikoa ya Shinyanga na
Tabora kupitia mradi wa Kijana jitambue uliolenga kuwasaidia vijana hao kufikia ndoto zao.
Tukai amesema kuwa watoto wengi hususani wa kike wamekuwa miongoni mwa vijana waliokatisha ndoto zao kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata Mimba
na Mazingira Magumu ya familia wanazotoka hukuyasisitiza mashirika kuwa bado liko jukumu kubwa la kufanya ili kuhakikihsa vijana wanafikia ndoto zao.
Aidha Tukai amewataka wazazi na walimu kuahkikisha wanatimiza jukumu lao kwa kuwalea watoto wa kike ili waweze kufikia ndoto ambapo amesema Mh. Rais Dkt. Samia amewapa fulsa ya watoto wa kike waliokatisha ndoto zao kurudi shule hivyo ni jukumu la jamii kuunga juhudi hizo.
Tukai hakusita kukema vitendo vya wazazi wanaotembea na watoto wadogo kimapenzi hali ambayo inachangiwa na mmomonyoko wa maadili kwa jamii na kusema kuwa hayuko tayari kuona wakazi wa Nzega na Mikoa ya Shinyanga na Tabora wanakaistiha ndoto zao kwa tabia mbovu za walezi
"Mimi hili jambo siko tayri na endepo nitakubaini mzazi au mlezi unafanya vitendo hivyo nitakuwajibisha kadri iwezekanavyo"
Katika Hatua nyingine Tukai amepongeza hatua zilizofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la Care International kwa kushirkiana na FEMA Tanzania kwa kuwasaidia vijana hao waliokatisha ndoto zao na wale walioko shuleni kuhakikisha nao wanafikia ndoto zao ikiwemo elimu na mafunzo ya ujasiliamali,ambapo ameomba Program hiyo itaendelea basi waikumbuke mikoa hiyo miwili.
Suala la baadhi ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayofanya kazi za kuelimisha jamii na mengine kwenda kinyume kwa kuhamasisiha vitendo vya ushoga ameyaona na kuyataka yapishe katika wilaya ya Nzega
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi kutoka shirika la Care International Tanzania Bi Haika Mtui amesema shirika hilo limekua likiendesha mafunzo kwa vijana ili kuwajengea uwezo wa kujitambua na kujithamini.
“Kama shirika shughuri zetu zimelenga kumuangazia mwanamke na msichana ambapo ni zaidi ya asilimia 80 ya utekelezaji wetu, lengo kubwa ni kupunguza idadi ya vijana hasa wasichana walio katika hatari ya kuacha shule kwa sababu mbalimbali na pili kusaidia vijana ambao wameacha shule kurudi tena shuleni au wapate shughuri zenye staha ili waendeshe maisha yao” amesema Haika Mtui Mkurugenzi Care International.
Mtui amesema katika kuwajengea uwezo wanawake na wasichana shirika hilo linazingatia misingi kadhaa ikiwemo kujiamini na uthubutu, elimu ya afya ya uzazi na jinsia, kumiliki rasilimali za uzalishaji na ujuzi wa kufanya biashara n kupata masoko ili kuhakikisha wanawajengewa mazingira wezeshi waweze kujisimamia maisha yao wenyewe pamoja na kujikinga na ukatili mbalimbali wa kijinsia.
Bi Mtui amesema kuwa Care International imekuwa ikitekeleza mradi mbalimbali ikiwemo ya kilimo,uchumi, uhifahdi wa mazingira na afya ya jamii ambapo imekuwa kwenye utekelezaji wake katika Mikoa 11 kwa kushirikiana na wadau wakuu ambao ni halmashauri mbalimbali kutoka kweye mikoa ya Shinyanga, Tabora, Tanga,Iringa, Njombe Arusha, Dodoma, Manyara Kilimanjaro Morogoro, Lindi, Mtwara Rukwa, Dar es salaam Tanga,Mbeya, Kigoma na Zanzibar ambapo miradi hiyo imekuwa tija kwa walengwa.
Meneja mradi wa ‘Kijana Jitambue’ kwa mkoa wa Tabora na Shinyanga Bw. Fravian Ligwa amesema mradi huo umesaidia elimu na malezi kwa vijana hao kutoka katika mikoa hiyo.
“Mradi huu ulianza January 2021 na kufikia ukomo March 2023 ambapo umekuwa na tija kubwa kwa vijana kwani umewajengea uwezo walimu waweze kutumia mbinu bora za ufundishaji darasani na pili kujenga uwezo kwa vijana ili waweze kujitambua na kufanya maamuzi sahihi na tatu ni kuhamasisha jamii kuwekeza kwenye masuala ya elimu ili waweze kusaidia vijana wao”, amesema Fravian Ligwa.
Nao baadhi ya wanafunzi waliopatiwa mafunzo hayo akiwemo Nana Kisumo na Eva Lucas wameshukuru mafunzo hayo kupitia mradi wa Kijana Jitambue umekuwa Msaada kwao kwa kuwa walikuwa wamepoteza ndoto zao hivyo matumaini na imani ya kufikia ndoto zao yamrejea.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai akizungumza na Wanafunzi vijana na baadhi ya wadau wa Mtoto kutoka Mikoa ya Shinyanga na Tabora mara baada ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiamini Vijana hao kupitia mradi wa "Kijana Jitambue."Wanufaika wa Mradi wa Kijana Jitambue kutoka Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kufunga mafunzo.
Post a Comment