" MADEREVA 109 WAKOSA SIFA, WAFUTIWA MADARAJA YA LESENI

MADEREVA 109 WAKOSA SIFA, WAFUTIWA MADARAJA YA LESENI

Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi, Justine Masejo amesema zoezi hilo ni la hiari hadi Aprili 30, 2023 likihusisha madereva wenye leseni zenye madaraja ambayo ni maalumu kwa ajili ya kubeba abiria pamoja na mizigo.

Amesema madereva wote wenye leseni zisizokuwa na sifa hasa wanaondesha magari ya abiria na mizigo lakini pia kwa wale ambao tayari wamefutiwa madaraja yao kwenda kusoma udereva katika vyuo vya Serikali katika kipindi kilichobaki.

Aidha amebainisha  kuwa baada ya kipindi hicho cha hiari kupita watafanya msako mkali kwa madereva wote waliokaidi ukaguzi huo na kwamba madereva wote pamoja na watumiaji wa vyombo vya moto wametakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea kutokana na ajali.

Post a Comment

Previous Post Next Post