
leo Jumapili tarehe 02.04,2023 Misa ya Dominika ya Matawi katika Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga inaendeleo.
Misa hiyo inaongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu.
Kwa mujibu wa Katibu wa Askofu Padre Paul Mahona, Misa hiyo imeanza saa 2:00 Asubuhi, na kuhudhuriwa na waamini kutoka maeneo mbalimbali ya Parokia ya Ngokolo.
Padre Mahona pia amebainisha kuwa, Askofu Sangu ataongoza maadhimisho yote ya juma kuu ambayo ni Misa ya Alhamisi kuu, Ibada ya Ijumaa kuu, Mkesha wa Pasaka na Misa ya Jumapili ya Pasaka kwenye makao makuu ya Jimbo, katika Kanisa kuu la Ngokolo .
Post a Comment