Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA) katika Jimbo Katoliki Shinyanga wamewapata viongozi wapya wa jimbo, kupitia uchaguzi uliofanyika katika Parokia ya Ilumya iliyopo wilayani Busega mkoa Simiyu.
Amewataja wengine kuwa ni Baraka Edward kutoka Parokia ya Buhangija ambaye amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa VIWAWA jimbo la Shinyanga, ambapo Joseph Mayunga kutoka Parokia ya Shy-Bush amechaguliwa kuwa Katibu.
Aidha Felister Boniventure kutoka Parokia ya Mtakatifu Luka-Bariadi amechaguliwa kuwa Katibu msaidizi VIWAWA Jimbo, ambapo Christina Zacharia kutoka Parokia ya Luguru amechaguliwa kuwa Mweka hazina.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Walei Jimbo Eustace Mgawe ambaye alikuwa Msimamizi wa uchaguzi huo, aliwapongeza VIWAWA wote kwa kufanya uchaguzi kwa uhuru,uwazi na utulivu na kwamba, viongozi waliochaguliwa wanapaswa kuwa watiifu kwa Kanisa na kwenda kuwaongoza wenzao katika kuinjilisha kupitia utume wa vijana.
Amewaomba kuangalia namna ambayo kupitia utume wao wanaweza kuwainua kiuchumi vijana wenzao.
Uchaguzi wa viongozi wa VIWAWA ngazi ya Jimbo hufanyika kila baada ya miaka mitatu, ukitanguliwa na chaguzi ngazi ya Parokia.

Post a Comment