Na Stela Paul, Misalaba Blog
Hayo
ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana April 15,2023 na Meneja Mahusiano wa Mgodi huo
Bernard Mihayo wakati akikabidhi fidia za samani za ndani kwa baadhi ya
waathirika hao ikiwemo pikipiki, baiskel, chakula, mashine za umwagiliaji,
vitanda pamoja na magodoro.
Amesema
waathirika 294 kati ya 304 wameshalipwa fidia zao ambapo zoezi hilo litaendelea
mpaka pale watakapokamilisha ulipaji wa fidia hizo.
" Tulikuwa na watu 304 na tayari
tumeshawalipa watu 294 na hao ni katika upotevu wa mali aina mbalimbali ikiwemo
ardhi, lakini kwa kaya kama hizi za leo wao walipoteza ardhi pamoja na nyumba,
"Kwa kuongezea waliopoteza nyumba,
tutaanza mchakato wa kujenga nyumba zao Mwezi wa sita nyumba kama 47, na
ukiangalia fidia yote mpaka Jana tumeshalipa shilingi bilioni 1 na milioni 800
na tunaendelea kulipa fidia. Na hiyo si pamoja na nyumba, nyumba zitakuwa na
gharama yake tofauti" amesema
Mihayo.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Bi.
Grace Mwandu amesema halmashauri imelipokea zoezi hilo kwa moyo wa dhati, huku
akiwasihi waathirika wa tope kutumia fidia zao kwa ustawi bora wa maisha.
"Tumelipokea vizuri zoezi hili kwa
sababu wananchi wote wamelizika na hakuna hata mmoja ambaye amekuwa na malalamiko
dhidi ya mgodi huu, zaidi tu kwa wananchi ambao wamelipwa watumie fidia hizo
kwa manufaa" amesema
Grace.
Kwa
upande wao wenyeviti wa vijiji vilivyoathirika na tope hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyeze
Revocatus Kulwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Ng'wanholo William Kabisi wamepongeza
jitihada mbalimbali ambazo zimefanywa na Mgodi huo ili kuhakikisha wananchi hao
wanapata fidia zao ambapo pia
wamethibitisha kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri.
Nao
baadhi ya wananchi waliolipwa fidia hizo wamepongeza na kuushukuru uongozi wa
Mgodi wa Almas wa Williamson Mwadui kwa kutekeleza kwa wakati zoezi la ulipaji
fidia.
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Almasi Mwadui
Benard Mihayo (kushoto) akikabidhi Fidia ya Jenereta kwa waathirika wa bwawa la
tope la mgodi huo.

Post a Comment