" MIILI YA WAUMINI 21 WALIOFUNGA MPAKA KUFA YAFUKULIWA NA POLISI KENYA

MIILI YA WAUMINI 21 WALIOFUNGA MPAKA KUFA YAFUKULIWA NA POLISI KENYA

 



Jeshi la Polisi nchini Kenya wamefukua miili ya watu 21 ambao ni waumini wa kanisa la News International Church, ambao inadaiwa wamefariki dunia kwa njaa baada ya kufuata maelekezo ya mchungaji wao ya kufunga mfululizo.

Mchungaji Paul Makenzie Nthenge ndiye anayedaiwa kuwapa maelekezo hayo waumini wake, ikidaiwa kwamba aliwaambia wakifunga mfululizo, wataenda kuonana ana kwa ana na Yesu.

Tayari mchungaji huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini humo huku taarifa zikieleza kwamba huenda makaburi mengine yakabainika.

Credit: DW

Post a Comment

Previous Post Next Post