" CR BELOUIZDAD USO KWA USO NA AL AHLY KLABU BINGWA BARANI AFRIKA.

CR BELOUIZDAD USO KWA USO NA AL AHLY KLABU BINGWA BARANI AFRIKA.

Na Elisha Petro, Misalaba Media

Klabu bingwa barani Africa (CAF) inarejea hii leo Ijumaa tarehe 16/02/2024 saa nne kamili usiku (10:00 PM) kwa mchezo wa kundi D wenyeji CR Belouizdad kuwakaribisha Al Ahly katika dimba la Stade du 5 Juillet 1962, al- jazair nchini Algeria.

CR Belouizdad wanaingia katika mchezo huo wakiwa nafasi ya tatu baada ya kukusanya alama nne  kwenye michezo yao mitatu waliyocheza, wameshinda mchezo mmoja dhidi ya Young Africa (3-0) ,sare mchezo mmoja dhidi ya Al Ahly (0-0)  na kupoteza mbele ya Madeama SC kwa goli (2-1 ).

Al Ahly wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama tano kwenye michezo mitatu waliyocheza,wameshinda mechi moja dhidi ya Medeama SC (3-0), sare michezo miwili dhidi ya Young Africa (1-1) na CR Belouizdad (0-0).

Mchezo mgumu kwa timu husika na kundi kwa ujumla kama CR Belouizdad wakishinda wao wataongoza kundi kwa alama 7 na kama Al Ahly akishinda atazidi kujitengenezea mazingira bora ya kufuzu  robo final na kuwaweka majaribuni CR Belouizdad katika mechi yao ya ugenini  dhidi ya Yanga SC.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post