Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu amewakumbusha wakristo kusimama imara katika imani yao, hasa wakati wa mahangaiko ya kimwili na kiroho, ili wanapoyaacha maisha ya hapa duniani wakaurithi uzima wa milele.
Askofu Sangu ameyasema hayo wakati akitoa mahubiri yake katika Misa ya Mazishi ya Mzee Elias Noninhale Malimi, ambaye ni Baba Mzazi wa Paroko wa Parokia ya Sayusayu Padre Paul Nhindilo, yaliyofanyika jana Ijumaa tarehe 23.02.2024, katika Kijiji cha Lubugu Parokia ya Ilumya, Wilayani Busega mkoani Simiyu.
Askofu Sangu amebainisha kuwa, imani ya Wakristo imekuwa ikiingia katika majaribu makubwa wakati wa mateso ma mahangaiko mbalimbali, ambapo wengi hushindwa kuvumilia na kuangukia kwa Shetani.
Amewaasa Wakristo kutoteleka kiimani kwa namna yoyote pale wanapokutana na changamoto yoyote na badala yake waendelee kumtumainia Mwenyezi Mungu na kuwa tayari wakati wote ili watakapofariki wakutwe wakiwa ndani ya Kristo na kuurithi uzima wa milele walioutumainia.
Amewaasa kuendelea kumwombea Mzee Elias Noninhale ili Mungu ampokee katika makazi yake ya milele kupitia imani aliyokuwanayo ambayo alifanya bidii kubwa kuwarithisha watoto wake hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa Padre Paul Nhindilo kutoka katika Familia yake.
Mzee Elias Noninhale alizaliwa mnamo Julai 1 mwaka 1936 katika kijiji cha Ilulu Mkoani Mwanza na kupata elimu yake ya Msingi kuanzia 1951 hadi 1954 katika shule ya Msingi Kiloleli.
Alijiunga na shule ya kati (Middle School) ya Ilumya kuanzia 1956 hadi 1957.
Katika maisha yake ya ndoa, alijaliwa kupata watoto 14 ambapo sita miongoni mwao ni watoto wa kike na wengine wanane ni wakiume.
Alifariki dunia mnamo Februari 19 mwaka huu katika Hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando Jijini Mwanza, kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua tangu mwaka 2021.
Mungu ailaze mahali pema Mbinguni roho ya Marehemu Mzee Elias Noninhale Malimi Amina

Paroko wa Parokia ya Mipa Padre Francis Kamani akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mzee Elias kabla ya adhimisho la Misa

Paroko wa Parokia ya Old Shinyanga Padre Daniel Kweja akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mzee Elias kabla ya adhimisho la Misa

Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mzee Elias Noninhale kabla ya adhimisho la Misa takatifu



Mapadre wakiwa kwenye maandamano kuelekea eneo la Misa

Askofu Sangu akiwa kwenye maandamano kuelekea eneo la Misa


Msomaji wa historia fupi ya marehemu mzee Elias

Wanakwaya wakiwa kwenye adhimisho la Misa


Waombolezaji wakiwa kwenye adhimisho la Misa


Waombolezaji wakifuatilia mahubiri ya Askofu Sangu


Mapadre wakiwa kwenye adhimisho la Misa



Wakili Askofu Padre Kizito Nyanga akitoa salamu za rambirambi kwa ndugu na waombolezaji wote kwa niaba ya Askofu

Mwenyekiti wa umoja wa Mapadre (UMAWATA) Jimbo la Shinyanga akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Mapadre

Viongozi mbalimbali wakitoa salam za rambirambi





Paroko wa Parokia ya Sayusayu Padre Paul Nhindilo akitoa neno la shukrani kwa Askofu Sangu,Mapadre,WATAWA na waombolezaji kwa kushiriki katika Misa ya mazishi ya Baba yake


Askofu Sangu akiongoza Sala ya buriani




Askofu Sangu akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mzee Elias Noninhale

Wakili Askofu Padre Kizito Nyanga akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu

Mapadre wakitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa marehemu





Mashemasi wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu .


WATAWA wakiaga mwili wa marehemu


Waombolezaji wakiendelea kuuaga mwili wa marehemu .



Wajukuu wa mzee Elias wakiwa wameubeba mwili kuelekea kaburini kwa mazishi

Askofu Sangu akiongoza Ibada ya Mazishi



Waombolezaji wakiuweka mwili wa mzee Elias kaburini


Askofu Sangu akiweka mchanga kwenye kaburi

Askofu Sangu akifukiza ubani kwenye kaburi


Waombolezaji wakiweka mchanga kwenye kaburi

Askofu Sangu akiweka Msalaba kwenye kaburi

Ndugu wa marehemu wakiweka Mashada katika kaburi



Askofu Sangu akiweka Shada katika kaburi la mzee Elias

Askofu Sangu akitoa neno na baraka kwa waombolezaji baada ya mazishi

Post a Comment