Na Mapuli Kitina Misalaba
Chama cha Skauti Manispaa ya Shinyanga leo Jumamos
Februari 24,2024 kimeadhimisha kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani huku
kikiwasihi wazazi na walezi kuwaruhusu watoto kujiunga na chama hicho ili
kuendeleza uzalendo wa Taifa.
Skauti hao wa Manispaa ya Shinyanga leo wamefanya
matembezi pamoja na kupanda miti zaidia ya Mia moja katika mtaa wa Miti mirefu
karibu na Soko la Mboga mboga mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani.
Naibu kamishna wa Skauti Wilaya ya Shinyanga Mwalimu Veronica Marwa amewataka vijana wa
Skauti kuendelea kuziishi kanuni za Skauti kuanzia ngazi ya familia ili
kuendeleza Taifa lenye uzalendo.
“Ninawaombeni vijana wangu tuendelee kuziishi kanuni za
uskauti tunasema kwamba Skauti ni mwaminifu na ni mtu wa kuaminiwa kwahiyo
tuanzia katika ngazi ya familia uaminifu tukiujenga kuanzia ngazi ya familia na
jamii kwa ujumla tutatengeneza Taifa lenye uzalendo wa hali ya juu kupitia
uzalendo kupitia uzalendo wetu kwa namna mbalimbali kujitoa, kujituma, maadili,
uajibikaji tutatengeneza Taifa lenye maendeleo na misingi inayokubalika katika
Nchi yetu”.amesema Marwa
Naibu kamishna huyo Mwalimu Veronica Marwa ametumia nafasi hiyo
pia kuwasisitiza vijana kujiepusha kufanya mambo yasiyofaa ambayo hupelekea
mmomonyoko wa maadili katika jamii ambapo amewahimiza wanafunzi kusoma kwa
bidii huku akiwaomba wazazi na walezi kuwaruhusu watoto kujiunga na Skauti.
“Lika lenu bado mko mashuleni kupitia uskauti wetu naomba
tuwe mfano bora kwa wanafunzi wengine tuhakikishe tunasoma kwa bidii kwa sababu
ipo imani kwa baadhi ya wazazi wanaona kwamba uskauti huwa una wafanya vijana
kuwa wazembe katika masomo yao niwatie moyo tuendelee kupambana darasani
tufanye vizuri ili kuondoa hiyo imani ya baadhi ya watu kudhani mnapoteza muda
wengine tumeona wenzenu wanazuiwa na wazazi kujiunga kwenye Skauti na kushiriki
kwenye shughuli mbalimbali za Skauti, niwaombe wazazi tuwaruhusu watoto
kujiunga na Skauti pia tuwaruhusu kushiriki kwenye maadhimisho mbalimbali
tunapowahitaji”amesema Marwa.
Aidha Mkufunzi wa Skauti Manispaa
ya Shinyanga Ernest Ngaramba ameiomba jamii kuilinda na kuitunza miti iliyopandwa
leo na Skauti ili iweze kustawi na vizuri kama sehemu ya kumbukumbu.
“Tumepanda miti ambayo haipungui mia moja hiyo miti tumepanda
kwa sababu tunathamini sana umuhimu wa miti katika jamii kwahiyo miti hiyo
tuliyoipanda itakuwa na faida sana katika jamii ikiwemo vivuli lakini pia miti
inasaidia katika upatikanaji wa mvua, tunachohitaji ni viongozi na jamii
inayozunguka eneo hilo kuendelee kuitunza isife”.amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa
wa miti mirefu ambaye pia ni Mwenyekiti wa wenyeviti Manispaa ya Shinyanga
Bwana Nassor Warioba ameahidi kusimamia miti iliyopandwa leo ili iweze kufikia
malengo ya serikali kupitia kampeni ya upandaji miti.
“Niwapongeze sana Skauti Manispaa ya Shinyanga kwa kupanda
miti siku ya leo na mimi nitahakikisha wanaozunguka eneo hilo wanaitunza ile miti
tutashirikia na afisa mazingira kwenda kuwapa utaratibu wa kuitunza ile miti
ili iweze kustwi vizuri”.amesema Mwenyekiti
Warioba
Chama cha Skauti Manispaa ya Shinyanga kimeungana na
watu wengine Duniani kote leo kuadhimisha kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani.
Robart Baden Powell ndio
jina la muanzilishi wa Skauti Duniani, Alizaliwa Februari 22, 1857 katika mitaa
ya Paddington london uingereza.
Robart Baden Powell alikuwa katika jeshi la kiingereza alifanya kazi katika jeshi hilo mwaka
1876-1910, na kwamba alikuwa na cheo cha liutenant General ambapo Januari
8,1941 alifaliki Dunia akiwa na umri wa Miaka 83 katika jimbo la Nyeri British
Kenya.
Skauti ni chama cha
hiyari cha kielimu kinachotowa mafunzo kwa vijana wote bila ubaguzi wa
rangi,jinsia,dini wala kabila kupitia mafunzo mbalimbali wanayoyapata kwenye
mfumo wa vikosi.
Malengo ya Skauti
ni kumuandaa kijana kiroho,kimwili,kimtazamo na kijamii ili aweze
kujitegemea,kusaidi,kuwajibika na kufaa kwa jamii.
Matembezi ya Skauti Manispaa ya Shinyanga
yakifanyika kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani.
Matembezi ya Skauti Manispaa ya Shinyanga
yakifanyika kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani.
Naibu kamishna wa Skauti Wilaya ya Shinyanga Mwalimu Veronica Marwa akitoa maelelezo namna
bora ya kupanda mti.
Naibu kamishna wa Skauti Wilaya ya Shinyanga Mwalimu Veronica Marwa akipanda mti leo
Jumamos Februari 24,2024 kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya
mwanzilishi wa Skauti Duniani.
Post a Comment