" KAMPUNI YA JAMBO GROUP YAING'OA GSM UDHAMINI MKUU NDANI YA PAMBA JIJI FC

KAMPUNI YA JAMBO GROUP YAING'OA GSM UDHAMINI MKUU NDANI YA PAMBA JIJI FC


Na Elisha Petro, Misalaba Media

Kampuni ya Jambo Food Product imefanikiwa kurejea kuidhamini Klabu ya Pamba Jiji FC (Wanakawe Kamo) yenye makazi yake jijini Mwanza baada ya kuing'oa Kampuni ya GSM na kusaini mkataba wa mwaka mmoja ( 2025/2026) kuwa Mdhamini Mkuu wa Klabu hiyo.

Hafla ya utiaji saini imefanyika leo, Septemba 13, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa kampuni hiyo, ambapo viongozi wa Kampuni ya  Jambo Group wameahidi kushirikiana kwa karibu na Pamba Jiji FC ili kuifikisha klabu hiyo katika malengo na mafanikio makubwa zaidi.

Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Group Bw. Nickson George, amesema lengo la udhamini huo ni kuimarisha ushirikiano na nembo Pamba Jiji kwa kuwaunganisha mashabiki wote Kanda ya Ziwa na kuendelea kutangaza bidhaa zinazozalishwa na Kampuni ya Jambo Group.

 “Mkataba huu tumesaini kwa mwaka mmoja ili kuandika historia mpya na kuwaleta pamoja mashabiki wa Pamba Jiji ndani na nje ya nchi ambao mara nyingi wamekuwa wakigawanyika katika timu za  Simba na Yanga, pia tumelenga kunufaika na klabu hii kwa kuendelea kukuza Brand ya Kampuni yetu kwa kutangaza bidhaa mbalimbali tunazalisha ,” amesema Bwn.  George

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Pamba Jiji Bwn. Peter Juma Lehhet amebainisha kuwa udhamini huo ni mwanzo mpya wa safari ya mafanikio ya klabu ya Pamba Jiji FC.

“Tulikuwa pamoja huko nyuma lakini safari ya kupeleka timu mbele zaidi imetufanya kuona umuhimu wa kurudi kwa wadhamini wa nyumbani kutoka Kanda ya Ziwa, tumekubaliana kuhakikisha chapa ya Pamba Jiji inaimarika zaidi,” amesema  Lehhet.

Naye Mwenyekiti wa Menejimenti wa Pamba Jiji Bwn. Bhiku Kotecha amewashukuruviongozi wa Mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa MHE. Said Mtanda  kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha udhamini huo.

“Hakuna mtu anaweza kuwekeza kwenye timu ambayo haifanyi vizuri hivyo  basi, kuanzia viongozi,wachezaji mpaka benchi la ufundi lazima tuhakikisha timu inakuwa imara na kupata matokeo ya ushindi pia tunaushukuru  uongozi wa Mkoa wa Mwanza chini ya mkuu wetu wa Mkoa MHE. Mtandao kwa ushirikiano wao uliofanikisha hatua hii,” amesema Kotecha.

Klabu ya Pamba Jiji FC imeanza safari yake kuwafuata Namungo FC wauaji wa kusini kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara (NBC premier league) utakaochezwa September 18,2025 katika uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa Mkoani Lindi.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post