Na Lydia Lugakila MbeyaGloria Ipopo Mwamajemba, maarufu kama Mchina, ambaye ni mgombea udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Iwambi, Mbeya Mjini, amewataka viongozi wa CCM, Dkt. Tulia Ackson, mgombea ubunge wa Jimbo la Uyole, na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi, kutomuacha nyuma katika harakati za maendeleo wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.Mhe, Ipopo ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika Septemba 12 Septemba 2025, ambapo ameeleza umuhimu wa ushirikiano kati yake na viongozi hao ili kuleta maendeleo katika kata ya Iwambi.Amesema anajivunia kuwa na viongozi wanawake wawili, Dkt. Tulia na Mhandisi Maryprisca, ambao yeye anawataja kama mfano wa uongozi bora na heshima kwa taifa.Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa viongozi hao kumsaidia ili kufanikisha lengo la maendeleo kwa wananchi wa Iwambi.“Wana Iwambi kazi yenu ni kuniombea dua na sala ili mawasiliano kati yetu yawe bora, na kata yetu iwe mfano wa maendeleo,” alisema Mhe. Ipopo.Ameongeza kuwa tayari amesoma na kuelewa vizuri ilani ya CCM, na yuko tayari kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi wa Iwambi. "Ilani ya mwaka 2025-2030 imejipanga vizuri, na nitaifanya kazi kutoka kwenye karatasi hadi vitendo," alisisitizaMhe. Ipopo pia amewaomba wananchi kumchagua Dkt. Tulia na Patrick Mwalunenge, mgombea ubunge wa Mbeya Mjini, kwani viongozi hao wana malengo ya kuleta mabadiliko chanya.Kwa upande wake, Dkt. Tulia Ackson amesisitiza umuhimu wa kujua yaliyofanywa na CCM na viongozi wake katika kuleta maendeleo, na kuwataka wananchi waendelee kuwa na imani na chama hicho.Dkt. Tulia Ackson, mgombea ubunge wa Jimbo la Uyole, ameleeza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshakamilisha maandalizi ya kuwahudumia wananchi, ingawa anatambua kuwepo kwa changamoto katika suala la upatikanaji wa maji na kuwa sasa, suluhisho limeelekezwa katika miradi mikubwa inayoenda kupatikana."Taabu ya maji, msiwe na wasiwasi tatizo la maji hamtalisikia tena, matatizo ya afya ya akina mama wakati wa kujifungua ndiyo yaliyokuwa makubwa, lakini sasa nawaombeni mkachague Gloria Mwamajemba (Mchina) ili aendeleze kazi nzuri," alisema Dkt. Tulia.Aidha, amesisitiza kuwa ni wakati wa kushirikiana ili kufikia mafanikio."Utakayekata naye kumi, ndivyo utaota naye moto,” aliongeza, huku akiwakaribisha Bi. Gloria pamoja na Patrick Mwalunenge waenda katika moto wa maendeleo.Dkt. Tulia alikumbusha wananchi kwamba yote waliyoyaanza yataendelea na kwamba wale ambao hawajayashuhudia, wanapaswa kuwa na imani na CCM, wakimwamini Rais Samia Suluhu Hassan, na kwamba kwa uongozi wa Gloria na Mwalunenge, wataona yale waliyotamani.Hata hivyo, Dkt. Tulia amemtaka mgombea udiwani Gloria Ipopo kushika ilani ya CCM wakati wa kampeni zake ili aweze kuwaelewesha wananchi kuhusu mipango ya maendeleo kwa uwazi na ufasaha.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA




Post a Comment