Na Osama Mohamedi Chobo, KilwaMgombea ubunge wa Jimbo la Kilwa Kusini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Hasnain Dewji, amesema anaelewa kwa undani changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, na ameahidi kuzitatua kwa vitendo endapo atapewa dhamana ya kuliongoza jimbo hilo bungeni.Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Garden Masoko, wilayani Kilwa, Dewji alitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi kuwa ni pamoja na miundombinu duni ya barabara, malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha miradi ya maendeleo, na upatikanaji hafifu wa huduma ya maji safi na salama.> “Nazijua changamoto za Kilwa Kusini. Niko tayari kupambana kuhakikisha kero hizi zinazowakabili wananchi zinakuwa historia. Nataka wananchi wa Kilwa waishi kwa furaha na kwa staha,” alisema Dewji mbele ya umati wa wananchi na wanachama wa CCM waliohudhuria uzinduzi huo.Katika hotuba yake, Dewji alimueleza mgeni rasmi wa hafla hiyo, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Alhaji Hassan Jarufu, kuhusu umuhimu wa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.Aidha, aliwaomba wananchi wa Kilwa Kusini na wanachama wa CCM kuendelea kukipa imani chama hicho kwa kuwachagua viongozi wake katika ngazi zote — urais, ubunge na udiwani — ili kuhakikisha kuwa maendeleo yanapatikana kwa kasi zaidi kupitia mfumo wa uongozi unaoshirikiana kwa karibu, maarufu kama mafiga matatu.Kwa upande wake, mgeni rasmi Alhaji Hassan Jarufu alisema kuwa CCM imeendelea kutekeleza miradi mingi ya maendeleo nchini kote na kwamba kazi hiyo itaendelea kwa nguvu zaidi endapo wananchi wataendelea kukipa chama hicho ridhaa ya kuongoza.> “Tusikubali kugawanyika. Tukichagua viongozi wote kutoka chama kimoja hadi ngazi ya juu, utekelezaji wa miradi unakuwa rahisi na wa haraka. Haya ndiyo tunayoyaita mafiga matatu,” alisisitiza Jarufu.Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na mgombea ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia CCM, Mheshimiwa Kinjekitile G. Mwiru, pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali kutoka mkoa wa Lindi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA





Post a Comment