" WAFANYA BIASHARA MKOANI SHINYANGA WAITAKA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA SUKARI AMBAYO IMECHANGIA MFUMKO WA BEI

WAFANYA BIASHARA MKOANI SHINYANGA WAITAKA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA SUKARI AMBAYO IMECHANGIA MFUMKO WA BEI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baadhi ya wafanya Biashara wakiwemo mama lishe Wilayani  Kishapu Mkoani Shinyanga, wameitaka serikali kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto ya upungufu wa Sukari ambayo imechangia kuwepo mfumko wa bei.

Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na Misalaba Media  ambapo wameeleza kuwa hivi karibuni bei ya Sukari imepanda kutoka elfu 2800 hadi elfu nne (4000) kwa kilo moja na kwamba upatikanaji wake ni mgumu.

Wamesema hatua hiyo imechangia kupungua kwa wateja na kuathiri mapato katika Biashara zao za kila siku huku wakiiomba serikali kushughulikia changamoto hiyo haraka ili kuondoa usumbufu unaojitokeza.

Kaimu afisa Biashara Wilaya ya Kishapu Albano Mayuma amesema serikali imejipanga kuhakikisha inathibiti mfumko wa bei ya Sukari na kwamba wafanyabiashara wanaouza kinyume na maelekezo ya serikali watachukuliwa hatua kali za kisheria

“Hii changamoto imekuwa ni kubwa kuanzia kwa mfanyabiashara mkubwa hadi mdogo wanalalamika ukija kwa watumiaji hasa wa majumbani nao wanalalamikia suala la upatikanaji lakini pia mfumko wa bei, sisi kama serikali tumejiandaa kuhakikisha kwamba tunadhibiti huu mfumko na kuhakikisha kwamba upatikanaji wa Sukari unakuwepo walau kwa ile bei ambayo imeelekezwa na bodi ya Sukari lakini pia tunatoa rai kwa wafanyabiashara ambao wanapandisha bei ya Sukari na wengine wanaficha Sukari tunawataka wasifanye kitendo hicho maana ni kosa la kisheria tukiwabaini hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yao ikiwa ni pamoja na kuwapiga faini”amesema Mayuma

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post