" WAKRISTO NA JAMII WAKUMBUSHWA KUMSHIRIKISHA MWENYEZI MUNGU KATIKA MASUALA YA KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA.

WAKRISTO NA JAMII WAKUMBUSHWA KUMSHIRIKISHA MWENYEZI MUNGU KATIKA MASUALA YA KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Wakristo  na jamii kwa ujumla wametakiwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika masuala ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Hayo yamebainishwa na kikundi cha wainjilisti wa makanisa ya Africa Inland Church  Tanzania (AICT) Manispaa ya Shinyanga ambao wanaendelea na maombi maalum ya kuombea mambo mbalimbali ikiwemo ukatili na kuombea amani Nchini.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Martha Mayunga ambaye ni mama Mchungaji pamoja na Mwinjilisti Hosea Seronga pamoja na mambo mengine wamesema sambamba na kutoa taarifa za ukatili kwenye mamlaka husikia  ni vema kumshirikisha pia Mwenyezi Mungu katika maombi ya kila siku.

Katika mahubiri yake ya leo Mwinjilisti Salome Seronga amewakumbusha wakristo kuendelea kumtumaini Mungu katika Maisha ya kila siku bila kujali changamoto zinazojitokeza.

Wainjilisti wa makanisa ya  AICT Manispaa ya Shinyanga wamekuwa na utaratibu wa kufanya maombo maalum kila mwezi kuombea mambo mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini, Serikali na Taifa kwa ujumla ambapo leo maomba yamefanyika katika Kanisa la AICT Pastoreti ya Ngokolo.

Post a Comment

Previous Post Next Post