
ARUSHA: Watu 15 wamefariki Dunia katika ajali iliyohusisha Lori la
Mizigo (Semi Trailer) na magari madogo matatu iliyotokea katika eneo la
Ngaramtoni, Wilayani Arumeru, Februari 24, 2024, ambapo Jeshi la Polisi
limesema chanzo cha ajali bado hakijafahamika lakini taarifa za awali
zinaonesha Lori lilipoteza uelekeo
Kwa mujibuwa taarifa za
mashuhuda, Lori hilo aina ya Scania lenye namba za Usajili ZF 6778 lilikuwa
likionesha ishara Taa za Hatari likiwa katika mwendo mkali na baadaye kuyagonga
magari matatu ambayo ni Basi dogo la Abiria (Hiace), Basi la Shule ya New Vision
lililokuwa na Watumishi wa Shule na Gari lingine dogo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha, SACP Justine Masejo amesema kuna majeruhi kadhaa ambao wapo katika hali
mbaya, pia amewataka Wananchi kufika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru kutambua
Miili ya waliofariki pamoja na majeruhi katika ajali hiyo
Chanzo Jamii Forum.
Post a Comment