Na Mapuli Kitina Misalaba
Wakristo na jamii kwa ujumla wameshauriwa kujiwekea utaratibu wa kuwa na kumbukumbu za
matukio muhimu katika maisha yao ili kutengeneza maisha bora yajayo.
Hayo yamezungumzwa leo April 1,2024 na Mchungaji
Christian Kubena wa Kanisa la Tanzania
Assembless of God T.A.G Shinyanga,
wakati akihubiri kwenye ibada ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa
kanisa hilo Nchini.
Mchungaji Kubena amesema ni muhimu kila mmoja kujiwekea
utaratibu wa kuwa na kumbukumbu ya matukio muhimu ili kutengeneza maisha bora
yajayo.
“Leo
tumekuwa na maadhimisho haya ya Miaka 85 tangu tuanze, tukio hili linaweza kuwa
na tafsiri mbalimbali lakini iko tafsiri iliyoyakweli ambayo hii inathibitishwa
hata na mamlaka ya maandiko matakatifu ya neno la Mungu na ukisoma kitabu cha kumbukumbu la tolati
sura ya 16 mstari ya kwanza hadi wa 17 anaelezea pale, Mungu anatoa maelekezo
ya mambo ambayo watu hao wanapaswa kukumbuka”.
“Mwanadamu
anapokumbuka kila kumbukumbu ina nguvu kwa sababu kila jambo linalotokea kwenye
maisha ya mwanadamu huwa lina kusudi na linamajira kwa kusema hivyo kumbukumbu
ulizonazo juu ya matukio mengi ya maisha yako Mungu ameziruhusu zinaweza kuwa
ni fursa ya kuwa na kesho nzuri zaidi, mtu asiyekuwa na kumbukumbu au asiye
kumbuka mara zote huwa hawezi kupiga hatua za maendeleo mfano mzuri tu mtu anakumbuka
vile alivyoteseka kwenye familia yao Baba alifariki au Mama alifariki wakawa
yatima watoto hao wanapokuwa watu wazima hawawezi kuchezea mali”.amesema
Mchungaji Kubena
Akisoma taarifa iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa
la T.A.G Rehoboth Christian Centre -Shinyanga
katibu wa kanisa hilo Bi. Gilselda Kasili ameelezea historia fupi ya ambapo ametaja
mwenendo na maendeleo ya Kanisa hilo.
Ameeleza kuwa kanisa hilo limeendelea kuifikia jamii
ambapo limefanikiwa kutembelea magreza, hospitali pamoja na kuchangia damu
salama katika hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Miaka 85.
“Tanzania
Assemblies of God ni Kanisa lililosajiriwa tarehe 21/10/1981 chini ya sheria ya
societies ordinance yam waka 1954 na kupewa namba ya usajiri SO/ 6246, kanisa
hili lilitokana na uamsho mkubwa ulioanza huko mtaa wa AZUSA, California
(Marekani), mwanzoni mwa karne iliyopita ya ishirini”.
“Mwanzilishi
wa kanisa hili nchini Tanzania ni mmisionari ndugu Paul Deer Mwaka 1939 wakati
huo ikiitwa Tanganyika hapo ndipo hesabu za umri wa kanisa letu hapa nchini
zinapoanzia, hivyo kutupa uhalali wa kusherehekea miaka 85 ya uhai wa Tanzania
Assemblies of God Mwaka huu wa 2024”.
“Historia inatuonesha kuwa katika miaka ya
mwanzo kanisa lilisimamiwa na
wamishenari wa kimarekani,
wachungaji wa kiafrika wakati huo,
Yohana Mpayo (Marehemu) na Petros,
walikuwa maaskofu chini ya Assemblies of
God Mission”.
“Kanisa
liliendelea kuongozwa katika mfumo huo wa kuongozwa na wamisionari hadi mwaka 1967, na Mwaka huo wa 1967, uongozi wa
Assemblies of God Mission, uliamua kulikabidhi kanisa kwa uongozi wa wenyeji na
Mchungaji Immanuel Lazaro, alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza mtanzania wa
kuongoza Tanzania Assemblies of God (TAG)”. amesema Kasili
“Lengo
kuu la kuanzishwa kwa kanisa hili ni kuwafikia watu wote kwa injili iliyo hai, iletayo wokovu
na kuleta uamsho mkubwa wa Bwana wetu Yesu Kristo hapa nchini, kwa hapa
Mkoani Shinyanga liliingia Mwaka 1968 na
hadi Mwaka huu kanisa lina miaka 56 Mkoani hapa,
“Malengo ya kanisa hili ni kulitimiza kusudi
lililokuwepo ndani ya kristo la kuwafikia wengine, na hili kulitimiza hili
lengo tumeweza kulifikia kwa njia mbali mbali ikiwemo; makongamano,mikutano ya
injili, semina,ushuhudiaji wa mtu mmoja mmoja na wa nyumba kwa nyumba, njia ya
sinema.
“Tunatambua
kuwa Mungu ametuweka hapa kama kanisa ili kuleta mabadiliko chanya kiroho,
kiakili na kimwili kwa jamii inayotuzunguka. Kanisa kwa kushirikiana na Taasisi
isiyokuwa ya Kiserikali ‘Compasion International’, tunawahudumia watoto walio
katika mazingira magumu katika nyanja ya kiroho, kimwili, kijamii na kiakili.
Hadi mwaka huu 2024 kituo kimeishahudumia jumla ya Watoto 250”.
“Mbali na kituo hiki kanisa tumeendelea
kuifikia jamii inayotuzunguka kwa ajili ya kukutana na mahitaji yao ya kimwili
na kiroho pia, wa kipindi hiki cha miaka 13 ya moto wa uamsho tumefanikiwa
kutembelea Magereza, Hospitali pamoja na kuchangia damu salama katika hospitali
yetu ya Manispaa ya Shinyanga”.
“Kanisa letu linawafikia wengine kwa njia ya
mtandao ambapo tunarusha ibada zetu na huduma zetu mbalimbali kwenye mtandao wa
‘facebook’ na you tube ikiwa ni pamoja na ibada mubashara, lengo likiwa ni kuwafikia watu wengi na hasa watumiaji wa
mitandao hiyo ndani na nje ya Tanzania”. amesema Kasili
Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amelipongeza
kanisa hilo la T.A.G kwa hatua hiyo ya
mafanikio.
Pamoja na mambo mengine kanisa la Tanzania
Assembless of God (T.A.G) Rehoboth
Christian Centre -Shinyanga leo Aprili mos limefanya
maandamano ya amani na kuchangia damu salama ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo.
Mchungaji Christian Kubena wa Kanisa la Tanzania Assembless of God T.A.G
Rehoboth Christian Centre –Shinyanga
akihubiri kwenye ibada ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa
hilo nchini.
Katibu wa kanisa la T.A.G Rehoboth Christian Centre -Shinyanga
Bi. Gilselda Kasili akisoma taarifa fupi ya kanisa hilo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mstahiki Meya
wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza leo Aprili
mos ambapo amelipongeza kanisa hilo la T.A.G kwa hatua hiyo ya mafanikio.

Kanisa la Rehoboth
Christian Centre lililopo mjini Shinyanga likiendelea na
maadamano ya amani ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo la T.A.G Nchini.

Kanisa la Rehoboth Christian Centre lililopo mjini Shinyanga likiendelea na maadamano ya amani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo la T.A.G Nchini.
Nyimbo mbalimbali za kusifu zikiendelea katika kanisa
la Rehoboth Christian Centre lililopo mjini Shinyanga
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo la T.A.G
Nchini.

wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko na kanisa kwa ujumla
wakiingia kanisa kwa ajili ya ibada maalum ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu
kuanzishwa kwa kanisa hilo.

Ibada maalum ya maadhimisho ya Miaka 85 tangu
kuanzishwa kwa kanisa la T.A.G nchini, ikiendelea mjini Shinyanga.

Post a Comment