Ticker

6/recent/ticker-posts

MTOTO WA MIAKA MIWILI AMWAGIWA MAJI YA MOTO MANISPAA YA KAHAMA MKOANI SHINYANGA

 

NA NEEMA NKUMBI HUHESO 

Mtoto wa miaka miwili jina tunalo mkazi wa mtaa wa Shunu kata ya Nyahanga manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga amelazwa katika hospitali ya manispaa hiyo kwa madai kuwa amemwagiwa maji ya moto na baba yake wa kambo anayejulikana kwa jina la Simon Hamisi.

Akisimulia tukio hilo mama mzazi wa mtoto huyo Elizabeth Mathias mbele ya wandishi wa habari katika wodi alikolazwa mtoto huyo amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa mbili usiku alipokuwa akichemsha maji jikoni ndipo mumewe alianzisha mzozo na kulipiga teke jiko ambalo lilikuwa na sufuria la maji ya moto na kummwagikia mtoto wake ambaye alikuwa amekaa karibu na jiko hilo.

Aidha Mwanamke huyo amesema kuwa tukio hilo linatokana na ulevi na kufafanua kuwa mumewe hajawahi kufanya tukio lolote baya kwa mwanae alimpenda sana lakini anashangaa kwa kilichotokea.

Mzazi huyo anaiomba serikali kumpa msaada wa matibabu kwani pesa aliyokuwa nayo ametumia kununua dawa na haijatosheleza matibabu pia mume wake tayari ameshikiliwa na polisi.

"Tangu tumekuja ustawi wa jamii humu mwanangu amechomwa sindano moja tu zingine mpaka hela nami sina bora wanisaidie mwanangu apone suala la kula nitahangaika kuwatafuta ndugu zangu wa mwanza", amesema mwanamke huyo.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo pia amelaani kitendo cha wazazi kutumia ulevi kufanya matukio ya kikatili.

Post a Comment

0 Comments