Ticker

6/recent/ticker-posts

WATIWA HATIANI KWA KUFANYA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA URASIMISHAJI MAKAZI

 Mnamo tarehe 05/07/2024 imetolewa hukumu ya kesi ya Jinai namba CC.386 /2024 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Gloria Nkwera, katika shauri lililoendeshwa na Mawakili Waandamizi wa Serikali – Veronica Chimwanda na Fatuma Waziri ambapo Ahmed Waziri Msika na wenzake 3 walitiwa hatiani kwa kosa la ubadhirifu na Ufujaji kinyume na kifungu Cha 28(2) Cha PCCA [Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022].

Shtaka lilikuwa ni kwamba, wakiwa viongozi wa Kamati ya Urasimishaji Makazi eneo la Kipunguni “A” katika Halmashauri ya Jiji la DSM, walifuja shilingi milioni kumi (10,000,000/-) zilizokuwa zimekusanywa na wananchi kwa ajili ya urasimishaji wa makazi yao.

Washtakiwa walifanya makubaliano (Plea bargaining) na wamelipa fedha hizo Serikalini na kuamriwa kutokufanya makosa yanayofanana na waliyoshtakiwa nayo kwa kipindi cha miaka 3.

Post a Comment

0 Comments