Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Allan Masanja akifungua mkutano mkuu Agosti 20,2024.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Wajumbe wa
mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa
Shinyanga leo Agosti 20,2024 wamekutana katika ukumbi wa mikutano wa Liga
Hotel, Manispaa ya Shinyanga, kujadili masuala mbalimbali yanayolenga
kuimarisha chama hicho na kuboresha ustawi wa wafanyakazi wa umma katika mkoa
huo.
Mkutano huo, ambao hufanyika kila baada ya Miaka
miwili na nusu, wajumbe kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa Shinyanga
wamehudhuria.
Katibu wa
TUGHE Mkoa wa Shinyanga Bwana. Ramadhan Pangara, amesoma taarifa ya utendaji wa
chama kwa kipindi cha kuanzia Oktoba 2021 hadi Julai 2024, akieleza kuwa chama
hicho kwa sasa kinajivunia kuwa na jumla ya wanachama 1,702.
“Mkoa
wa Shinyanga kwa sasa tuna wanachama 1,702. Hii ni kutokana na juhudi za
kuongeza wanachama wapya na pia kupungua kwa idadi kutokana na sababu
mbalimbali, ikiwemo kustaafu hata hivyo, tutaendelea kuongeza idadi ya
wanachama na kuboresha huduma kwa wanachama wetu,”
amesema Pangara.
Katibu huyo amebainisha mafanikio ya chama katika
utetezi wa wafanyakazi, akieleza kuwa TUGHE Mkoa wa Shinyanga imeweza kutoa
huduma za utetezi kwa watumishi 25 walioshtakiwa kwa makosa ya nidhamu, huku
wanne wakiendelea kupatiwa huduma za kisheria katika mashauri ya jinai.
“Tumefanikiwa
kurudisha kazini watumishi watatu, na pia tumehamasisha waajiri kutoa zawadi za
wafanyakazi bora kwa wakati tutaendelea kutoa elimu kwa wafanyakazi ili kuepuka
matukio yanayopelekea kuchukuliwa hatua za nidhamu na jinai,”
amesema Katibu Pangara.
Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Allan
Masanja, amesisitiza umuhimu wa wajumbe wa mkutano huo kutekeleza majukumu yao
kwa uadilifu na kuwahamasisha watumishi wa umma kufuata sheria, kanuni, na
taratibu za nchi.
Amewahimiza wajumbe kuwa mstari wa mbele katika
kupambana na rushwa mahali pa kazi, akiamini kuwa mkoa wa Shinyanga unaweza
kuweka rekodi nzuri katika vita dhidi ya rushwa.
“Msisahau
kuzungumzia rushwa mahala pa kazi si kuzuia migogoro tu, rushwa ni mbaya hasa
mahali pa kazi nina imani tutavunja rekodi kwa mkoa wa Shinyanga kwa mwaka huu
na miaka ijayo, tusiwe na mtumishi ambaye anatuhumiwa kwa rushwa na ukiukwaji
wa kanuni na taratibu za watumishi wa umma,” amesema Dkt.
Masanja.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati za Wanawake wa
TUGHE Mkoa wa Shinyanga, Experantia Misalaba, ameeleza kuwa kamati hiyo imebuni
miradi mbalimbali yenye lengo la kuinua hali ya kiuchumi ya wanachama, ikiwa ni
pamoja na vikundi vya vikoba vinavyosaidia wanachama kujikopesha kwa riba nafuu
ili kuepuka mikopo yenye riba kubwa.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga Catherine Masalu amehitimisha
kwa kuwahimiza watumishi wengine, hususan wale wapya, kujiunga na chama hicho
ili kunufaika na huduma na mikakati ya chama.
Mkutano mkuu wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga umehitimishwa kwa wajumbe kuahidi kuendelea
kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuwasisitiza watumishi wote kushirikiana
kwa karibu ili kuimarisha utendaji na kuepusha migogoro kazini.
Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Allan Masanja
akizungumza kwenye mkutano mkuu TUGHE Agosti
20,2024.
Katibu wa
TUGHE Mkoa wa Shinyanga Bwana. Ramadhan Pangara akisoma taarifa ya kazi ya
chama kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Oktoba 2021 hadi Julai 2024 Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa
TUGHE Mkoa wa Shinyanga Bwana. Ramadhan Pangara akisoma taarifa ya kazi ya
chama kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Oktoba 2021 hadi Julai 2024 Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa
TUGHE Mkoa wa Shinyanga Bwana. Ramadhan Pangara akisoma taarifa ya kazi ya
chama kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Oktoba 2021 hadi Julai 2024 Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati za Wanawake wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga, Experantia Misalaba akizungumza kwenye mkutano mkuu Agosti 20,2024.
Mwenyekiti wa Kamati za Wanawake wa TUGHE Mkoa wa
Shinyanga, Experantia Misalaba akizungumza kwenye mkutano mkuu Agosti 20,2024.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga Catherine Masalu akizungumza
kwenye mkutano mkuu Agosti 20,2024.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga Catherine Masalu akizungumza kwenye mkutano mkuu Agosti 20,2024.
Post a Comment