" WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA CRDB, AZITAKA BENKI KUIUNGA MKONO BENKI YA CRDB KUWAKOPESHA WACHIMBA MADINI

WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA CRDB, AZITAKA BENKI KUIUNGA MKONO BENKI YA CRDB KUWAKOPESHA WACHIMBA MADINI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, ameipongeza Benki ya CRDB kwa juhudi zake za kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kwa mikopo yenye masharti nafuu, akizihimiza benki nyingine kuiga mfano huo ili kuongeza mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa.

Ameyasema hayo leo Jumatatu Agosti 19,2024 akiwa mgeni rasmi kwenye  kikao cha kupokea ripoti ya Benk ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wajimbaji wa kati na wadogo ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano Planet Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Ameipongeza  Benki ya CRDB kwa hatua zake madhubuti katika kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kwa mikopo yenye masharti nafuu.

Waziri Mavunde ameelezea kufurahishwa kwake na jinsi benki hiyo ilivyotekeleza maelekezo aliyoyatoa mwaka jana kwa benki mbalimbali, akisisitiza kwamba mfano huo unapaswa kuigwa na taasisi nyingine za fedha.

Mhe. Mavunde amekumbusha kuwa wachimbaji wadogo ni kundi muhimu katika uchumi wa madini nchini, lakini wanakabiliwa na changamoto ya mtaji.

mwaka jana kwa watendaji wa benki za biashara nchini.

"Wachimbaji wadogo ni jeshi kubwa kwenye sekta ya madini nchini, lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya mtaji Benki kama CRDB zimeonyesha njia kwa kutoa kipaumbele kwa watu hawa hii ni hatua muhimu katika kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa,"

“Iwapo benki zingine zitafuata nyayo za CRDB, sekta ya madini itaendelea kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya taifa letu,” amesema Mavunde.

Pia Waziri Mavunde ametumia nafasi hiyo kufafanua  kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya uchimbaji, ikiwemo kuwezesha wachimbaji wadogo kupata elimu na ujuzi wa kufanya utafiti wa maeneo yenye madini kwa usahihi zaidi kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Afisa Mkuu wa Biashara wa CRDB, Boma Raballa, ameangazia juhudi za benki hiyo kwa kueleza kuwa wameanzisha kitengo maalum cha madini ambacho kinawasaidia wachimbaji wadogo kupata mikopo haraka na kwa masharti nafuu.

“Mpaka sasa tumeshakopesha zaidi ya shilingi bilioni 64 kwa sekta ya madini, ambapo shilingi bilioni 19 zilienda kwa wachimbaji wadogo,” amesema Raballa.

Waziri Mavunde ameendelea kwa kusisitiza umuhimu wa benki zingine kuunga mkono juhudi hizi, akiamini kuwa kwa kufanya hivyo, mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa utaongezeka maradufu.

Katika kikao hicho, Waziri Mavunde amekabidhi mfano wa hundi kwa wachimbaji wa Kanda ya Ziwa, wakisisitiza dhamira ya Serikali na Benki ya CRDB katika kuimarisha sekta ya madini nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amesisitiza umuhimu wa sekta ya madini ambapo amesema Mkoa wa Shinyanga umechangia asilimia 85 ya maduhuli ya sekta ya madini kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024  huku akisisitiza kuwa upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo utaimarisha uchimbaji na kuongeza mapato ya serikali.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Masache Kasaka, ameongeza kwa kuipongeza Wizara ya Madini na taasisi zake kwa juhudi zao za kuleta mageuzi katika sekta ya madini, akieleza kuwa mageuzi haya ni sehemu ya maelekezo ya Kamati hiyo katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata mikopo kwa urahisi.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania (FEMATA), John Wambura Bina, naye ameipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya madini, ambapo amesema uwekezaji huu umeanza kuleta tija na umewezesha wachimbaji wadogo kukopesheka kutokana na uwepo wa mashine za uchorongaji zinazosaidia kupata taarifa sahihi za uwepo wa madini.

Benki ya CRDB ni mojawapo ya benki zinazoongoza Afrika Mashariki, ikitoa huduma mbalimbali za kifedha kwa wateja wadogo, wa kati, na wakubwa, Benki hiyo inatambulika kimataifa kwa uimara wake, ikiwa na daraja la juu la uimara (B1) kutoka Moody’s Investors Service. CRDB pia ni benki bora Tanzania kwa miaka kadhaa, ikitoa huduma kwa zaidi ya wateja milioni 4 kupitia mtandao wake mpana wa matawi na CRDB Wakala.

CRDB imekuwa kiungo muhimu cha biashara katika nchi za Tanzania, Burundi, na DRC, ikiwa na mtandao mpana wa zaidi ya matawi 260, CRDB Wakala 25,000, mashine za manunuzi 1,800, na Kituo cha Huduma kwa Wateja kinachotoa huduma saa 24/7.

Benki hii ni ya kwanza nchini Tanzania kutambuliwa na Moody’s Investors Service, kampuni ya kimataifa ya utafiti, kama moja ya benki 10 imara na salama Afrika katika uwekezaji.

Pia, Benki ya CRDB imepata utambuzi wa Mfuko wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UN Green Climate Fund) tangu mwaka 2019 na imetambuliwa kama benki bora Tanzania na majarida ya Global Finance na Euromoney.

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika leo Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika leo Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika leo Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akielezea hatua kadhaa zilizofanywa na benki katika kuwawezesha wachimbaji wadogo pamoja na changamoto ilizokutana nazo.Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akiendelea kuelezea hatua kadhaa zilizofanywa na benki katika kuwawezesha wachimbaji wadogo pamoja na changamoto ilizokutana nazo.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika leo Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika leo Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akitoa salamu wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akitoa salamu wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Kamishna wa Madini nchini, Dkt. Abdulrahman Mwanga akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe. Hussein Kassu akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini Mhe. Masanche Kasaka akizungumzawakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.

Meneja Mwandamizi wa Dawati Maalumu la Madini la Benki ya CRDB, Abdulrahim Msonde akiwasilisha mada ya mikopo ya biashara na vitendea kazi

Meneja Mwandamizi wa Dawati Maalumu la Madini la Benki ya CRDB, Abdulrahim Msonde akiwasilisha mada ya mikopo ya biashara na vitendea kazi
 Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na wa kati wa Benki ya CRDB, Agness Kisinini akitoa akiwasilisha mada inayosema wachimbaji na ukopeshaji.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post