WAZIRI wa Madini
Anthony Mavunde ametembelea Mgodi wa Almasi Mwadui (WDL) uliopo Wilayani
Kishapu Mkoa wa Shinyanga na kukumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo kushuka
kwa soko la Almasi duniani.
Ziara hiyo aliyoifanya leo Agosti 19,2024 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wizara ya madini, pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge nishati na madini.
Amesema changamoto ya kushuka kwa soko la madini ya Almasi ni ya dunia nzima siyo Mwadui pekee,hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na Mgodi wa Almasi Mwadui katika utatuzi wa changamoto hiyo ili kurudisha heshima na hadhi ya madini ya Almasi.
"Kushuka kwa soko la madini ya Almasi inasababishwa na sababu kuu nne ,moja ikiwa ni kuwapo kwa uzalishaji wa madini ya Almasi za Maabara," amesema Mavunde.
"Kushuka kwa soko hili la Almasi hata sisi Serikali ambao tuna ubia na mgodi huu tutakosa mapato, na tuta hakikisha tunashirikiana na mgodi kuitatua ili kurudisha heshima na hadhi ya madini ya Almasi," ameongeza Mavunde.
Aidha,ametoa maagizo kwa Mgodi kwamba kwa wale watoa huduma ndani ya mgodi huo(Local Content) wakae nao na kuwaeleza hali halisi ya kushuka kwa soko la Almasi na siyo kuwapunguza bila kuwapatia taarifa.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amesema Serikali ya Mkoa humo itaendelea kushirikiana na wawekezaji, huku akisisitiza suala la uzalendo hasa kwenye ulipaji wa mapato ya serikali.

Post a Comment