Bara la Afrika limejaaliwa kuwa na mila na desturi nyingi ambazo zinafahamika na zingine ambazo hazifahamiki kwa ulimwengu mzima, nyingi kati ya mila hizo ambazo hazifahamiki zinapatikana katika sehemu za ndani sana na zisizofikika kirahisi.
Zifuatazo ni mila na desturi tano ambazo si za kawaida zinazofanywa na baadhi ya makabila barani Afrika.
Kuiba mke kwenye ngoma za usiku Mila hii inatekelezwa na kabila ndogo la Wodaabe linalopatikana kati ya kaskazini mwa Nigeria, kusini mwa nchi ya Cameroon, magharibi mwa Afrika ya Kati na kusini mwa nchi ya Chad ambapo wakati wa sherehe za kimila, jamii hiyo hujumuika katika ngoma za usiku. Na katika usiku huo wanaume wanaruhusiwa kuiba mwanamke yoyote na kwenda kustarehe naye hadi asubuhi bila kujali mwanamke huyo ameolewa ama la!, isipokuwa mwanamke mwenyewe akikataa . Kupima urijali wa bwana harusi Tamaduni hii inapatikana nchini Uganda kwenye kabila la Banyankole, ambapo shangazi wa bibi harusi mtarajiwa hushiriki tendo la ndoa na bwana harusi ili kupima kama mwanaume huyo ni rijali kabla ya harusi haijafungwa. Makabila mengine nchini humo hulazimika kusikiliza dirishani wakati bwana na bibi harusi wakishiriki tendo la ndoa. Kuruka kundi la ng’ombe Nchini Ethiopia, kijana kabla hajafuzu kuingia katika hatua hiyo hupimwa kwa kupewa jaribio la kukimbia na kuwaruka kundi la ng’ombe ambao wamepangwa katika mstari akiwa uchi, tukio linalojulikana kwa jina la ‘Hamar’ ambapo baada ya kumaliza, marafiki wa kike wa kijana huyo humponya majeraha yake kwa mafuta kisha hucheza ngoma na kufurahi pamoja.
Kuvumilia kipigo ili kupata mke na heshima Kwenye jamii ya fulani nchini Benin, wanaume ambao wanahitaji kuanzisha familia hawana budi kuvumilia kipigo kutoka kwa wazee wa jamii hiyo endapo upande wa mwanamke utachagua utaratibu huo unaojulikana kama ‘ Sharo’ . Endapo mwanaume atashindwa kuvumilia kipigo hicho basi taratibu za harusi hiyo zitavunjwa na inakuwa ni aibu kubwa kwake na familia yake.
Sherehe za mazishi Katika taratibu za mazishi za kabila la Chewa nchini Malawi, hufanya utaratibu wa siri unaojulikana kama ‘Nyau’ ambapo hufunika nyuso zao kwa maski wakati wa mazishi. Huanza kwa kuuosha mwili wa marehemu kwa kuumwagia maji kisha hayo maji ambayo yanaoshewa maiti hutumika kwa kutengenezea chakula ambacho huliwa na watu wote wanaohudhuria katika mazishi hayo.
Tunapokea watoto kwa ajili ya Nursery na Primary kwa mwaka wa masomo 2024/2025.
Ada kwa Muhula:
- Nursery: 150,000/=
- Primary: 210,000/=
Usafiri na hosteli zinapatikana.
Shule ipo Basihaya-Dawasco.
Mawasiliano:
0714 927 246
0766 927 247
Nafasi ni chache sana!
ADSTERRA
OFA KUBWA YA MAFUNZO YA UOKAJI BIASHARA MWANZA NA KANDA YA ZIWA
WASILIANA NASI 0788 774 594 au 0715 224 264
OFISI YA MARIASUZY BAKERY EXPERT (SME)
Inakuletea OFA KUBWA ya mafunzo ya uokaji na uendeshaji wa biashara kwa mkoa wa Mwanza na kanda ya ziwa.
Mafunzo haya yanalenga kukupa ujuzi na mbinu bora za uokaji pamoja na usimamizi wa biashara zako ili kuhakikisha unafanikiwa katika sekta ya ujasiriamali.
Tarehe: Kuanzia 28 Oktoba 2024 hadi 1 Novemba 2024
Muda: Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 10:00 Jioni
Mahali: Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza
Ada:Shilingi 125,000 kwa siku 5
Malipo: Yafanyike kupitia akaunti ya Azania Bank, A/C: 001810427389 – Mary Malemi.
NB: Nafasi 10 za bure zinatolewa kwa walemavu.
Kwa mawasiliano zaidi:
Simu: 0788 774 594 au 0715 224 264
Usikose nafasi hii ya kipekee ya kuongeza ujuzi wako na kuimarisha biashara yako!
0 Comments