Ticker

6/recent/ticker-posts

IFAHAMU HISTORIA YA PAROKIA YA MTAKATIFU JOHN BARIADI JIMBO KATOLIKI SHINYANGA.


Parokia ya Mtakatifu John Bariadi ilianza kama Kigango cha Parokia ya Old Maswa chini ya Padre Paul Fagan mwaka 1960 kikiitwa Kigango cha Somanda huku Misa na Ibada zilikuwa zikifanyika chini ya mti wa Mkuyu uliopo Parokiani hapo.

Mnamo mwaka 1967 Kanisa dogo lilijengwa kwa ajili ya kuabudia ambalo lipo mpaka hii leo ikiwa ni ukumbi mdogo wa Parokia uliopo pembeni na jukwaa la nje la Parokia hiyo.

Mwaka 1983 hadi 1985 Kanisa kubwa lilijengwa kutokana na ongezeko la Waamini ambapo tarehe 15.05.1984 aliyekuwa Askofu wa kwanza mzalendo  wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Askofu Castory Sekwa  alitoa tamko la Kigango cha Somanda  kuwa Parokia huku mwaka 1987 Kanisa hilo lilitabarukiwa na aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Askofu Castory Sekwa.

Mwaka 2021 Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu alitoa maelekezo ya ukarabati wa Kanisa hilo ili kuendana na maendeleo ya Kanisa na Mkoa ambapo tarehe 10.02.2022 ukarabati huo ulianza rasmi na kukamilika mwaka 2024.

Tarehe 26.09.2024 Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu aliongoza Misa takatifu ya Kutabaruku Kanisa hilo baada ya ukarabati huo kukamilika na kutoa Sakramenti takatifu ya Kipaimara kwa waimarishwa 172 wa Parokia ya Mtakatifu John Bariadi.







Post a Comment

0 Comments