Na Mapuli Kitina Misalaba
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi
mkubwa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni katika
jimbo la Shinyanga Mjini, kwa kujinyakulia mitaa 55, vijiji 17, na vitongoji 83
kati ya jumla ya vitongoji 84 vilivyoshindaniwa.
Kwa mujibu wa matokeo
yaliyotangazwa, CCM imepata ushindi wa asilimia 99.3, huku Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) kikibeba nafasi moja pekee kwenye kitongoji kimoja, sawa
na asilimia 0.7 ya kura zote.
Katika kata mbalimbali za Shinyanga
Mjini, matokeo yalionyesha nguvu kubwa ya CCM, ikiwemo:
- Kata ya Ngokolo (mitaa 7)
- Ndala (mitaa 5)
- Kambarage (mitaa 6)
- Old Shinyanga (vitongoji 13)
- Ibadakuli (vitongoji 21, huku CCM ikibeba 20 na CHADEMA
1).
Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe.
Paschal Katambi, amewashukuru wakazi wa Shinyanga kwa imani yao kubwa kwa CCM
na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuwaletea maendeleo endelevu.
"Asanteni wanashinyanga
nawaahidi maendeleo zaidi” amesema Katambi.
Kwa ujumla, uchaguzi wa mwaka huu umeonyesha
dhamira ya wananchi ya kuendelea kuamini Chama Cha Mapinduzi katika kusimamia
maendeleo ya Shinyanga.
Post a Comment