Na Mapuli Kitina Misalaba
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA), amefunga Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini leo Februari 14, 2025 huku akitoa wito kwa watangazaji kutumia lugha fasaha na yenye maadili katika kazi zao.
Katika hotuba yake, Mwana FA ameeleza kuwa hadi sasa vyombo vya utangazaji vilivyosajiliwa nchini ni 517, vikiwemo vituo vya redio 233, televisheni 68, televisheni za mtandaoni (online TV) 206 na redio za mtandaoni 10.
Amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kuzingatia weledi katika utangazaji, hususan matumizi ya Kiswahili sanifu ili kuboresha mawasiliano na kuhamasisha maendeleo ya jamii.
Mkutano huo umefanyikia jijini Dodoma ambapo umehudhuriwa na wadau wa sekta ya habari kutoka mikoa mbalimbali, wakijadili changamoto na fursa zinazoikabili tasnia hiyo katika dunia ya sasa ya kidijitali.
Picha ya pamoja

















Post a Comment