Kituo cha kulelea watoto wadogo mchana Angel Gabriel Day Care Center kilichopo Mwasele Manispaa ya Shinyanga, kimefanya ziara maalum ya kielimu kwa watoto wake, kwa lengo la kuwafundisha kwa njia ya vitendo kupitia mpango maalum uliopewa jina la “ANGEL GABRIEL LEARNING BEYOND CLASSROOM.”
Kupitia mpango huo, watoto wamepata fursa ya kujifunza nje ya mazingira ya kawaida ya darasani, kwa kutumia milango yao mitano ya fahamu: kuona, kusikia, kugusa, kuonja na kuhisi. Ziara hiyo iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya Jambo Group of Companies iliwapa watoto maarifa mapya na kuwaongezea furaha.
Mambo muhimu yaliyojiri kwenye ziara hiyo ni pamoja na:
✅ Kutembelea Supermarket ya Jambo – Watoto wamejifunza kwa vitendo namna bidhaa mbalimbali huwekwa na kununuliwa katika soko la kisasa. Hii imewasaidia kuelewa tabia za ununuzi na aina za bidhaa.
✅ Kutembelea Kiwanda cha Jambo – Watoto waliona kwa macho yao jinsi bidhaa wanazopenda kama juisi, keki, mikate na ice cream zinavyotengenezwa. Uzoefu huu uliwapanua uelewa kuhusu mchakato wa uzalishaji wa bidhaa hizo kuanzia kiwandani hadi madukani.
✅ Ziara ya Jambo Zoo – Watoto wamekutana uso kwa uso na wanyama mbalimbali waliokuwa wanasoma darasani kwa nadharia. Uzoefu huu umewasaidia kuunganisha maarifa ya kitabu na uhalisia.
✅ Chakula cha Mchana Level One – Watoto wamefurahia mlo wa mchana katika mazingira mapya na rafiki kwa mtoto, wakifurahia vyakula mbalimbali vilivyopikwa kwa ubora wa hali ya juu.
✅ Picha za Kumbukumbu (Photoshoot) – Watoto na walimu wamepiga picha nyingi kwa pamoja ili kutunza kumbukumbu za siku hiyo maalum.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Bi. Damary Mollessi, amesema kuwa lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuwasaidia watoto kujifunza kwa kuona na kufanya, ili kuwajengea msingi thabiti wa maarifa ya maisha.
“Tunafundisha kwa njia ambazo mtoto anajifunza kirahisi. Tunawaandaa kuuelewa ulimwengu waliopo sasa na ule wanaouelekea kadri wanavyokua,” amesema Mollessi.
Angel Gabriel Day Care ni kituo kilichosajiliwa rasmi na serikali na kina mazingira rafiki kwa ukuaji wa mtoto, ikiwa na walimu waliobobea katika malezi na elimu ya awali.
Kwa wazazi wanaotafuta mahali salama na bora kwa watoto wao, Angel Gabriel Day Care inakaribisha watoto kujiunga kwa muhula wa pili unaoanza tarehe 8 Julai 2025.
Kaulimbiu ya kituo: “Making your child's world better.”
Kwa mawasiliano zaidi:
📞 0752 516 753 / 0675 969 213
📍Mwasele, Shinyanga
Mkurugenzi wa kituo hicho cha Angel Gabriel Day Care, Bi. Damary Mollessi ametumia nafasi hiyo kushukuru na kupongeza uongozi mzima wa Jambo Group of Companies kwa mapokezi mazuri, huduma bora na ukarimu wa hali ya juu kwa watoto hao katika kila eneo walilotembelea.
Post a Comment