“Hadi kufikia Machi 2025, deni la Taifa lilifikia shilingi trilioni 107.7 kutoka shilingi trilioni 91.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 14.9. Kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilikuwa shilingi trilioni 34.76 na deni la nje lilikuwa shilingi bilioni 70.94. Ongezeko la deni lilitokana na Serikali kuendelea kupokea mikopo mipya kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji”, – Prof. Kitila.
Sehemu ya hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26, bungeni jijini Dodoma, Alhamisi Juni 12, 2025
Post a Comment