" Simba Wako Tayari Kwa Mchezo wa Dabi Jumapili…

Simba Wako Tayari Kwa Mchezo wa Dabi Jumapili…

 

” …Yeah Maandalizi yanaendelea vizuri kuelekea mchezo wetu wa Jumapili na kikubwa kabisa ni kwamba…kuna baadhi ya wachezaji ambao walikuwa na changamoto ndogo…Kama mtakumbuka mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Singida Black Stars tulocheza Manyara wachezaji wawili walipata Changamoto…

Mmh…Camara alipata Changamoto kidogo ya Kifua na ameweza kurejea kwenye mazoezi na yuko timamu kabisa…Yuko cleared medically kurejea kuitumikia timu…

mchezaji mwingine ilikuwa ni Nouma(Valentin) ambaye alipata changamoto ya Goti…naye pia tumeshaweza kum-clear, hivyo ameweza kurudi kwenye mazoezi…

Aah…Mchezaji mwingine Che Malone alikuwa na changamoto naye lakini ameweza kurejea kama mlivyokuwa mkimuona katika mechi kadhaa za nyuma kwa dakika kadhaa lakini sasa hivi status yake ni nzuri sana, availability yake itakuwa sahihi kabisa kutumika kwa dakika zote…

Pamoja na mchezaji wa nne ambaye ni Mzamiru Yassin ambaye hakuonekana kwa muda mrefu sana, naye ameshaweza kurejea kwenye kikosi kwa maana ya kufanya mazoezi kwa muda wote na wengine(Group Training)…

Kifupi ni kwamba tuna kikosi cha wachezaji karibia wote ambao wako tayari kwa ajili ya mchezo na…so tunafahamu maandalizi yanakwenda vizuri na hatujapata changamoto in between na natarajia tutamaliza maandalizi yetu haya vizuri kwa kuwa na availability ya wachezaji wote (Katika mchezo v Yanga SC Juni 15)…”

Post a Comment

Previous Post Next Post