" Halima Mdee: Mimi Bado nipo CHADEMA, Wasiponihitaji Nitatafuta pa Kwenda

Halima Mdee: Mimi Bado nipo CHADEMA, Wasiponihitaji Nitatafuta pa Kwenda

 Halima Mdee

Halima Mdee

Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee amesema yeye bado ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @chadematzofficial mpaka hivi sasa na yupo tayari kuendelea Kufanya kazi na chama hicho.

Akihojiwa na vyombo vya habari leo jijini Dodoma Mdee amesema
“sijaondoka CHADEMA mpaka sasa sijajua mambo yatakayokuja kutokea mbele so far kwa mwanasiasa yoyote anatamani kupata room ya kufanya siasa na mimi naamini kwamba anayeweza akaziba room ya mtu kufanya kazi ni mungu peke yake siyo binadamu”

Hata hivyo Mdee ameeleza kuwa kama chama hicho hakitompa nafasi ya kuendelea kufanya kazi zake za kisiasa kupitia chama hicho basi atatafuta ‘alternative’ (mbadala) huku akieleza kuwa hana hamu ya kukihama chama hicho.

Post a Comment

Previous Post Next Post