" KAMENGE ATIMIZA SEHEMU YA AHADI YAKE KKKT USHARIKA BWANJAI MISSENYI

KAMENGE ATIMIZA SEHEMU YA AHADI YAKE KKKT USHARIKA BWANJAI MISSENYI


Na Mwandishi wetu MISSENYI

Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Bwanjai, Wilayani Missenyi, mkoani Kagera, wamempongeza Evance Kamenge kwa uaminifu aliouonyesha katika kutimiza ahadi yake aliyoiahidi katika kanisa la Bwanjai KKKT juu ya uzinduzi wa Albamu ya wanakwaya wa kanisa hilo.

Akizungumza kupitia hafla ya uzinduzi ya albamu ya kwaya ya kanisa hilo iliyofanyika Juni 15,2025 Kamenge ameonyesha kujitolea kwa njia ya pekee na kuthibitisha nafasi yake kama kiongozi wa mfano katika jamii.

Mwenyekiti wa usharika, ambaye alizungumza kwa niaba ya waumini, alieleza furaha yake kuhusu Kamenge kutimiza ahadi yake ya shilingi laki 5 kutoka shilingi milioni 2 kwa ajili ya maandalizi ya kurekodi video ya albamu ya kwaya.

Kamenge amesema kuwa ametoa shilingi laki 5 kama sehemu ya uhamasishaji huo ambapo mwenyekiti wa usharika huo amesema kuwa "ni watu wachache wanaoahidi na kutoa huku akionyesha kuwa Kamenge ni mfano wa uaminifu mbele za Mungu.

Naye Mchungaji wa kanisa la KKKT usharika wa Bwanjai, Gideon Mwesigwa Kayungi, amesisitiza kuwa Kamenge ni mtu mwenye nia safi na mfano bora na kuwa watazidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili ampe nguvu na kibali cha kuwa kiongozi bora wa baadae wakati anapoendelea kuonyesha uwezo wake na malengo yake yenye mafanikio.

 Mchungaji Mwesigwa ameongeza kuwa hatua aliyochukua Kamenge ni ya mfano wa kuigwa katika jamii huku akiwaomba watu wengine kuiga mfano huo.

Aidha Evance Kamenge, akiwa mgeni rasmi, ameeleza jinsi alivyopata mafanikio kupitia usharika wa KKKT Kigarama kata Kanyigo na kuwa anaami kusaidia usharika wa Bwanjai anakuwa amesaidia nyumbani.

"Nawapongeza kwa hatua hii, japo naumia kuona ibada ya mavuno inakuwa hivi," alisema Kamenge kwa huzuni huku akionyesha kuwa Wananchi wa wilaya ya Missenyi wana uzalishaji mdogo wa mazao yakiwemo ya ndizi, gonja na mahindi jambo ambalo ameahidi kulipambania ili kuona mabadiliko katika uzalishaji yeye kama mkulima na mchumi.

Ameongeza kuwa jina Kamenge linaashiria matumaini ya kuona mashamba mengi yakizalisha kwa wingi.

Mkulima na mchumi huyo amewaomba waumini na viongozi wa kanisa hilo hilo kuendelea kumuombea wakati anapopanga kwa sasa kugombea ubunge katika Jimbo la Missenyi. 

"Naamini kwa maombi yenu ninakwenda kutimiza ahadi yangu na kiu yangu kwa wana Missenyi, wanaKagera na Watanzania kwa ujumla," alisema Kamenge.

Ili kuhakikisha maendeleo ya kilimo katika Wilaya ya Missenyi, Kamenge amejitolea kuboresha hali ya maisha ya wakulima wa Missenyi na Kagera kwa jumla.

Hata hivyo Kamenge ameonyesha kuwa yuko tayari kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha mabadiliko chanya yanapatikana kupitia kilimo.


Post a Comment

Previous Post Next Post