" KATA YA MASANGA YANUFAIKA NA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 5.3 KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM KWA MIAKA MITANO, DIWANI ENOCK REUBEN BUNDALA ATOA TAARIFA

KATA YA MASANGA YANUFAIKA NA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 5.3 KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM KWA MIAKA MITANO, DIWANI ENOCK REUBEN BUNDALA ATOA TAARIFA

Zaidi ya shilingi bilioni 5.3 zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya Masanga, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 2021 hadi 2025.

Taarifa hiyo imetolewa na Diwani wa kata hiyo, Mhe. Enock Reuben Bundala, katika mkutano mkuu wa CCM kata ya Masanga, ambapo wananchi na viongozi wa chama na jumuiya zake ikiwemo jumuiya za UWT na UVCCM, na wanachama wa CCM wamehudhuria kusikiliza kusikiliza na kupokea taarifa ya utekelezaji wa ahadi za chama hicho tawala.

Kwa mujibu wa Diwani huyo, kata ya Masanga ni miongoni mwa kata 29 za Halmashauri ya Kishapu, ikiwa na vijiji saba, vitongoji 30 na kaya 2,062 zenye jumla ya wakazi 15,953, ambapo wanaume ni 7,918 na wanawake 8,035 kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ambapo shughuli kuu za wakazi wake ni kilimo, ufugaji na biashara.

Katika sekta ya elimu Mh. Enock amesema  mafanikio makubwa yameonekana kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule ambapo Shule ya sekondari Bulekela imenufaika kwa kiasi kikubwa, na kwamba vyumba saba vya madarasa vimejengwa na vingine saba kukarabatiwa, huku  yakijengwa madarasa mengine mawili, ofisi moja pamoja na madawati ambapo ujenzi huu umewezeshwa na nguvu ya wananchi pamoja na mchango kutoka Mfuko wa Jimbo.

Aidha, ameeleza kuwa shule ya msingi Buzinza imejengewa vyumba vitatu vya madarasa na vyoo vyenye matundu matatu huku shule ya msingi Hilishi, vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja vimejengwa, na tayari ujenzi wa nyumba ya mwalimu umeanza, japokuwa bado haujakamilika ambapo Shule ya msingi Isemo nayo imenufaika kwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi, huku shule ya msingi Mwajidalala ikikamilisha ujenzi wa madarasa mawili na ofisi.

Kwa upande wa shule ya msingi Ng’wanga’halanga, Diwani Mhe. Enock amesema kumekamilika ujenzi wa vyoo vyenye matundu saba, ambapo taasisi ya TCRS imetoa mchango mkubwa na kwamba Shule hiyo hiyo pia imenufaika na ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo wa lita 50,000 na vyoo vingine vya matundu nane.

Mhe. Enock katika taarifa yake amesema shule ya msingi Masanga, vyoo vyenye matundu 22 vimejengwa, pamoja na tanki jingine la maji la ukubwa kama huo, huku pia nyumba ya mwalimu ikiwa ni sehemu ya miradi iliyotekelezwa ambapo  Madawati zaidi ya 100 yametengenezwa kwa shule za msingi sita na sekondari moja, na shule shikizi mpya imeanzishwa katika kijiji cha Bulekela.

Amesema katika sekta ya afya, Kituo cha Afya Ng’wanga’halanga kimeboreshwa kwa kujengewa jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, na nyumba za watumishi. Pia vifaa tiba vimenunuliwa, pamoja na mashine ya kufulia, jenereta ya umeme, na gari la wagonjwa ambapo Zahanati ya Masanga imejengewa vyoo vya kisasa na kichomea taka, huku Zahanati ya Ng’wajidalala ikipatiwa vifaa vya umeme wa jua na kuunganishiwa rasmi.

Kwa upande wa maji Mhe. Enock ameeleza kuwa, kata ya Masanga imenufaika na mradi mkubwa wa maji ya bomba katika vijiji vya Masanga, Mwampalo na Ng’wanga’halanga. Aidha, usanifu wa visima vya maji umefanyika katika vijiji vya Dodoma, Buzinza, Ng’wajidalala na Bulekela.

Amesema katika sekta ya nishati, umeme umeunganishwa katika vijiji vya Dodoma, Buzinza, Mwajidalala na Bulekela ambapo Ofisi za vijiji vya Dodoma na Mwampalo zimejengwa chini ya Idara ya Utawala.

Wakati huo huo Mhe. Enock amesema upande wa miundombinu ya barabara pia umeshuhudia mafanikio kwa ujenzi wa barabara ya Mwajidalala kuelekea Manonga na barabara ya kona ya Teng’wa Makolo – Senta Mwajidalala ambapo Mnara wa mawasiliano ya Vodacom umejengwa katika kijiji cha Dodoma, hatua inayoboresha mawasiliano kwa wananchi wa maeneo hayo.

Katika sekta ya kilimo na ushirika, ghala la kununulia pamba limejengwa katika kijiji cha Mwajidalala na kwamba nyumba ya mtumishi wa kata imejengwa kusaidia watendaji waliopo. Vikundi vya ujasiriamali katika kata hiyo pia vimewezeshwa kupitia mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 138, ambapo vikundi 10 tayari vimeanza kurejesha mikopo hiyo pia amesema, kupitia TASAF, kiasi cha zaidi ya milioni 73 kimetolewa kwa wanufaika, wakiwemo wanafunzi.

Mhe. Bundala  ameeleza kuwa mafanikio haya yamewezekana kwa ushirikiano mkubwa kati ya viongozi, wananchi na wadau mbalimbali huku akipongezwa na wakazi wa kata hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi, na kwamba wananchi hao wameahidi kuendelea kumuunga mkono kisiasa na kimaendeleo.

Aidha, jumuiya ya UWT na UVCCM imezindua zoezi la kuchangia gharama za kuchukua na kurudisha fomu ya kugombea udiwani kwa diwani huyo katika uchaguzi ujao, ambapo zaidi ya taki mbili, mazao, mbuzi na ng’ombe zimepatikana kwa ajili ya siku hiyo maalum.

Diwani wa kata Masanga, Mhe. Enock Reuben Bundala, akizungumza kwenye mkutano mkuu wa kata ambao umelenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kata ya Masanga kwa kipindi cha Miaka mitano kuanzia Mwaka 2021 hadi 2025.

Diwani wa kata Masanga, Mhe. Enock Reuben Bundala, akizungumza kwenye mkutano mkuu wa kata ambao umelenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kata ya Masanga kwa kipindi cha Miaka mitano kuanzia Mwaka 2021 hadi 2025.

Diwani wa kata Masanga, Mhe. Enock Reuben Bundala, akizungumza kwenye mkutano mkuu wa kata ambao umelenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kata ya Masanga kwa kipindi cha Miaka mitano kuanzia Mwaka 2021 hadi 2025.

Diwani wa kata ya Mwamalasa Mhe. Bushi Salum Mpina akizungumza kwenye mkutano huo ikiwa mgeni mwalikwa.

Wanachama wa CCM kata ya Masanga wakiwa kwenye mkutano huo.

Diwani wa viti maalum akizungumza kwenye mkutano huo.


Wanachama wa CCM kata ya Masanga wakiwa kwenye mkutano huo.

Diwani wa viti maalum akizungumza kwenye mkutano huo.




 

Post a Comment

Previous Post Next Post