" SALAMU ZA EVANCE KAMENGE KWA WAKRISTO KATIKA MAADHIMISHO YA PENTECOST

SALAMU ZA EVANCE KAMENGE KWA WAKRISTO KATIKA MAADHIMISHO YA PENTECOST


Na Lydia Lugakila, Misalaba Media -Kagera

Kila mwaka, tarehe 8 Juni, Wakristo duniani kote huadhimisha siku ya Pentecost, siku ambayo inakumbusha kushuka kwa Roho Mtakatifu na kuanzishwa kwa Kanisa la Kristo. 

Katika maadhimisho haya matakatifu, Evance Kamenge, mchumi na mkulima kutoka mkoani Kagera, amewapongeza Wakristo wote kwa kutimiza siku hii yenye neema na umuhimu wa kiroho.

Pentecost ni siku ya kusisitiza nguvu ya Umoja, uzima wa Roho Mtakatifu, pamoja na wajibu wa kila mwanajamii kujenga jamii yenye upendo, maadili, pia mshikamano.

 Kamenge amesisitiza kwamba katika kipindi hiki, Wakristo wanatarajiwa kuwa mwangaza wa tumaini, si tu katika familia zao bali pia katika jamii na taifa kwa ujumla.

Aidha, Kamenge amewaomba Wakristo kuendelea kueneza upendo na umoja katika nyanja mbalimbali za maisha, akisisitiza kwamba kuungana kwao kunaweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii. 

Evance Kamenge amewakumbusha kwamba Roho Mtakatifu anaposhuka, anawakumbusha Wakristo wajibu wao wa kutenda mema na kuwa kielelezo cha nuru katika nyakati za giza.

Ameonge kuwa ni muhimu kwa Wakristo kuwa na mshikamano na kushirikiana katika kutekeleza malengo yao ya kiroho na kijamii.

katika maadhimisho hayo ya Pentecost, Kamenge anatoa wito kwa kila Mkristo kuwa na upendo na matumaini, na kujitolea kwaajili ya ujenzi wa jamii bora.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post