Zaidi ya shilingi bilioni 5.3 zimetumika kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya Masanga, Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, mkoani Shinyanga, katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 2021 hadi 2025.
Taarifa hiyo imetolewa na Diwani wa kata hiyo, Mhe.
Enock Reuben Bundala, katika mkutano mkuu wa CCM kata ya Masanga,
ambapo wananchi na viongozi wa chama na jumuiya zake ikiwemo jumuiya za UWT na UVCCM, na wanachama wa CCM wamehudhuria kusikiliza kusikiliza na kupokea taarifa ya utekelezaji wa ahadi za chama hicho tawala.
Kwa mujibu wa Diwani huyo, kata ya Masanga ni
miongoni mwa kata 29 za Halmashauri ya Kishapu, ikiwa na vijiji saba, vitongoji
30 na kaya 2,062 zenye jumla ya wakazi 15,953, ambapo wanaume ni 7,918 na
wanawake 8,035 kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ambapo shughuli
kuu za wakazi wake ni kilimo, ufugaji na biashara.
Katika sekta ya elimu Mh. Enock amesema mafanikio makubwa yameonekana kupitia ujenzi
na ukarabati wa miundombinu ya shule ambapo Shule ya sekondari Bulekela
imenufaika kwa kiasi kikubwa, na kwamba vyumba saba vya madarasa vimejengwa na
vingine saba kukarabatiwa, huku yakijengwa madarasa mengine mawili, ofisi moja
pamoja na madawati ambapo ujenzi huu umewezeshwa na nguvu ya wananchi pamoja na
mchango kutoka Mfuko wa Jimbo.
Aidha, ameeleza kuwa shule ya msingi Buzinza
imejengewa vyumba vitatu vya madarasa na vyoo vyenye matundu matatu huku shule
ya msingi Hilishi, vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja vimejengwa, na
tayari ujenzi wa nyumba ya mwalimu umeanza, japokuwa bado haujakamilika ambapo Shule
ya msingi Isemo nayo imenufaika kwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na
ofisi, huku shule ya msingi Mwajidalala ikikamilisha ujenzi wa madarasa mawili
na ofisi.
Kwa upande wa shule ya msingi Ng’wanga’halanga, Diwani
Mhe. Enock amesema kumekamilika ujenzi wa vyoo vyenye matundu saba, ambapo
taasisi ya TCRS imetoa mchango mkubwa na kwamba Shule hiyo hiyo pia imenufaika
na ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo wa lita 50,000 na vyoo vingine vya
matundu nane.
Mhe. Enock katika taarifa yake amesema shule ya msingi
Masanga, vyoo vyenye matundu 22 vimejengwa, pamoja na tanki jingine la maji la
ukubwa kama huo, huku pia nyumba ya mwalimu ikiwa ni sehemu ya miradi
iliyotekelezwa ambapo Madawati zaidi ya
100 yametengenezwa kwa shule za msingi sita na sekondari moja, na shule shikizi
mpya imeanzishwa katika kijiji cha Bulekela.
Amesema katika sekta ya afya, Kituo cha Afya
Ng’wanga’halanga kimeboreshwa kwa kujengewa jengo la mama na mtoto, jengo la
upasuaji, na nyumba za watumishi. Pia vifaa tiba vimenunuliwa, pamoja na
mashine ya kufulia, jenereta ya umeme, na gari la wagonjwa ambapo Zahanati ya
Masanga imejengewa vyoo vya kisasa na kichomea taka, huku Zahanati ya
Ng’wajidalala ikipatiwa vifaa vya umeme wa jua na kuunganishiwa rasmi.
Kwa upande wa maji Mhe. Enock ameeleza kuwa, kata ya
Masanga imenufaika na mradi mkubwa wa maji ya bomba katika vijiji vya Masanga,
Mwampalo na Ng’wanga’halanga. Aidha, usanifu wa visima vya maji umefanyika
katika vijiji vya Dodoma, Buzinza, Ng’wajidalala na Bulekela.
Amesema katika sekta ya nishati, umeme umeunganishwa
katika vijiji vya Dodoma, Buzinza, Mwajidalala na Bulekela ambapo Ofisi za
vijiji vya Dodoma na Mwampalo zimejengwa chini ya Idara ya Utawala.
Wakati huo huo Mhe. Enock amesema upande wa
miundombinu ya barabara pia umeshuhudia mafanikio kwa ujenzi wa barabara ya
Mwajidalala kuelekea Manonga na barabara ya kona ya Teng’wa Makolo – Senta
Mwajidalala ambapo Mnara wa mawasiliano ya Vodacom umejengwa katika kijiji cha
Dodoma, hatua inayoboresha mawasiliano kwa wananchi wa maeneo hayo.
Katika sekta ya kilimo na ushirika, ghala la
kununulia pamba limejengwa katika kijiji cha Mwajidalala na kwamba nyumba ya
mtumishi wa kata imejengwa kusaidia watendaji waliopo. Vikundi vya ujasiriamali
katika kata hiyo pia vimewezeshwa kupitia mikopo yenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 138, ambapo vikundi 10 tayari vimeanza kurejesha mikopo hiyo
pia amesema, kupitia TASAF, kiasi cha zaidi ya milioni 73 kimetolewa kwa
wanufaika, wakiwemo wanafunzi.
Mhe. Bundala ameeleza kuwa mafanikio haya yamewezekana kwa
ushirikiano mkubwa kati ya viongozi, wananchi na wadau mbalimbali huku akipongezwa
na wakazi wa kata hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi, na kwamba wananchi hao
wameahidi kuendelea kumuunga mkono kisiasa na kimaendeleo.

Diwani wa kata Masanga, Mhe. Enock Reuben Bundala, akizungumza
kwenye mkutano mkuu wa kata ambao umelenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa
ilani ya CCM kata ya Masanga kwa kipindi cha Miaka mitano kuanzia Mwaka 2021
hadi 2025.

Diwani wa kata Masanga, Mhe. Enock Reuben Bundala, akizungumza kwenye mkutano mkuu wa kata ambao umelenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kata ya Masanga kwa kipindi cha Miaka mitano kuanzia Mwaka 2021 hadi 2025.

Wanachama wa CCM kata ya Masanga wakiwa kwenye
mkutano huo.
Diwani wa viti maalum akizungumza kwenye mkutano huo.

Diwani wa kata Masanga, Mhe. Enock Reuben Bundala, akizungumza
kwenye mkutano mkuu wa kata ambao umelenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa
ilani ya CCM kata ya Masanga kwa kipindi cha Miaka mitano kuanzia Mwaka 2021
hadi 2025.

Diwani wa kata Masanga, Mhe. Enock Reuben Bundala, akitoa taarifa ya utekelezaji wa

Post a Comment