Na Mapuli Kitina Misalaba
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema itaendelea
kushirikiana na vyombo vya habari katika juhudi za kuwafikishia wananchi elimu
juu ya wajibu wao na namna ya kunufaika na huduma za nishati na maji.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 16, 2025 na Meneja wa
EWURA Kanda ya Mashariki, Nyirabu Musira, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa EWURA, kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu
mamlaka hiyo na majukumu yake na kwamba semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Beachcomber Hotel, jijini Dar es Salaam.
Musira amesema
ushirikiano kati ya EWURA na vyombo vya habari ni muhimu kwa kuwa waandishi
ndio daraja la kuifikia jamii, hivyo ni vema wakaelewa kwa undani kazi na
wajibu wa mamlaka hiyo ili waweze kuhabarisha kwa usahihi na kuelimisha
wananchi.
Semina hiyo imeandaliwa
na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN),
ikiwa na lengo la kuwaimarisha wanachama wake katika kutekeleza majukumu yao
kwa weledi na ufanisi.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa MISA-TAN, Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa kushirikiana na
taasisi hiyo, akieleza kuwa semina hiyo ni hatua muhimu ya kuimarisha mahusiano
baina ya EWURA na vyombo vya habari.
Soko ameongeza kuwa, waandishi waliopata elimu hiyo
wataweza kuandika habari zenye matokeo chanya na kusaidia kutatua changamoto za
nishati na maji katika jamii.
Akizungumza wakati wa
semina hiyo, Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma kutoka EWURA, Wilfred
Mwakalosi, ameeleza kwa kina kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo pamoja na
matarajio ya EWURA kwa waandishi wa habari katika kusaidia kuelimisha umma.
Naye Mjumbe wa Bodi ya
MISA-TAN, Alex Benson akisoma maazimio ya semina hiyo, amesema nimuhimu semina
kama hiyo kuendelea kufanyika kwa wanachama wa MISA-TAN katika mikoa yote ili
kuongeza uelewa kwa wanahabari kote nchini.
Makamu Mwenyekiti wa
MISA-TAN Roda Marumo amewahimiza waandishi waliopata elimu hiyo kwenda kuwa mabalozi
wazuri katika jamii, huku akiipongeza EWURA kwa kutoa mafunzo hayo muhimu kwa
tasnia ya habari.
Semina hiyo
imehudhuriwa na wanachama wa MISA-TAN kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza,
Arusha, Pwani, Dar es Salaam na Shinyanga, ambao wameahidi kutumia elimu
waliyoipata kwa vitendo, huku wakipata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa na
wataalamu kutoka EWURA.
Kwa pamoja, washiriki wameonesha ari ya kuwa sehemu
ya mabadiliko chanya katika sekta ya nishati na maji kupitia kazi zao za
uandishi wa habari.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya Mashariki akifungua semina hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa EWURA leo Juni 16, 2025.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na majukumu yake inaendelea leo katika ukumbi wa mikutano wa Beachcomber Hotel, jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo imefunguliwa rasmi na Nyirabu Musira kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, ambapo amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuelewa kazi na majukumu ya EWURA ili waweze kuhabarisha jamii kwa usahihi na ufasaha.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa hiyo hiyo, akisema kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano baina ya mamlaka hiyo na vyombo vya habari nchini.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ambao ni wanachama wa MISA-TAN kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Pwani, Dar es Salaam na Shinyanga, wameahidi kuzingatia yale wanayojifunza kupitia mawasilisho mbalimbali na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo katika kazi zao za kila siku za uandishi wa habari.
Semina hiyo inaendelea, ikilenga kuimarisha uelewa wa wanahabari juu ya mfumo wa udhibiti wa sekta ya nishati na maji nchini.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya Mashariki akifungua semina hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa EWURA leo Juni 16, 2025.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya Mashariki akifungua semina hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa EWURA leo Juni 16, 2025.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko akitaja malengo ya semina hiyo leo Juni 16, 2025.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko akitaja malengo ya semina hiyo leo Juni 16, 2025.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko akizungumza kwenye semina hiyo leo Juni 16, 2025.

Afisa
Uhusiano na Mawasiliano ya Umma kutoka UWURA, Wilfred Mwakalosi akielezea EWURA
na majukumu yake pamoja na matarajio ya EWURA kwa Waandishi.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma kutoka UWURA, Wilfred Mwakalosi akielezea EWURA na majukumu yake pamoja na matarajio ya EWURA kwa Waandishi.


Semina na kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuifahamu EWURA na majukumu yake, ikiendelea jijini Dar Es Salaam leo Jumatatu Juni 16, 2025 na kwamba imeratibiwa na MISA TAN.


Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, Alex Benson akisoma
maazimio ya semina hiyo leo Juni 16, 2025.Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, Alex Benson akisoma
maazimio ya semina hiyo leo Juni 16, 2025.
Makamu Mwenyekiti wa MISA-TAN Roda Marumo akizungumza
kwenye semina hiyo Juni 16, 2025.
Makamu Mwenyekiti wa MISA-TAN Roda Marumo akizungumza kwenye semina hiyo Juni 16, 2025.
Post a Comment