" MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI PASCHAL PATROBAS KATAMBI AKABIDHI ZAIDI YA BAISKELI 480 KWA VIONGOZI MBALIMBALI NA MASHINE 10 ZA KUTOTOLESHA KUKU KWA UWT SHINYANGA

MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI PASCHAL PATROBAS KATAMBI AKABIDHI ZAIDI YA BAISKELI 480 KWA VIONGOZI MBALIMBALI NA MASHINE 10 ZA KUTOTOLESHA KUKU KWA UWT SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Paschal Patrobas Katambi, akizungumza. 
Na Elisha Petro, Misalaba Media

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Paschal Patrobas Katambi, amekabidhi zaidi  ya baiskeli 480 kwa viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa  ya Shinyanga,mashine 10 za kutotolesha vifaranga vya kuku kwa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Wilaya  ya Shinyanga Mjini pamoja na vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza viongozi hao kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea kuufanya katika kutimiza majukumu yao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo  Mhe. Katambi amesema hatua hiyo ni sehemu ya shukrani kwa viongozi hao kwa ushirikiano wanaouonyesha katika kutimiza majukumu yao ambayo  yanaimarisha shughuli za chama katika ngazi za chini pamoja na kuwainua kiuchumi  wanawake kupitia miradi ya ufugaji wa kuku.

“Niwashukuru viongozi wetu kwa ushirikiano mnaouonyesha katika kutimiza shughuli za Chama chetu bila ushirikiano leo hii tusingekuwa hapa tulipo kwani maendeleo yoyote yale yanahitaji ushirikiano unatambua kuwa maendeleo ya chama ni lazima tushirikiane wote hongereni sana wazazi wetu na viongozi wote wakiwemo UWT kwa kazi kubwa mnayoe delea kuifanya baiskeli hizi nimewaletea ni za kwenu" alisema Katambi.

Aidha,Mhe. Katambi amewasisitiza wanawake wa UWT kutumia mradi wa kufugaji kuku ili kuendelea kufungua fursa za kiuchumi kupitia ufugaji.

"Ndugu zangu UWT mashine hizi ni sehemu ya mradi mzuri ambapo Kila mashine inauwezo wa kutotolesha vifaranga 200 kwa mara moja nawakabidhi leo mtaona namna mtakavyozitumia mashine hizi lakini huu ni mkakati wa kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi"

Kwa upande wao baadhi ya viongozi waliopokea baiskeli na viongozi wa  UWT waliopokea mashine za kutotolesha kuku  wamemshukuru Mhe. Katambi kwa moyo wa utoaji na kuahidi kutumia vifaa hivyo baiskeli  kwa lengo lililokusudiwa la kuleta tija kwa chama na jamii.






Post a Comment

Previous Post Next Post