
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule, akziungumza na waandishi wa habari leo Juni 13,2025 kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara kesho Juni 14,2025 jijini Dodoma ya kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa huo.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule, akziungumza na waandishi wa habari leo Juni 13,2025 kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara kesho Juni 14,2025 jijini Dodoma ya kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa huo.
Na.Meleka Kulwa-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja jijini Dodoma ya kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa huo.
Hayo yamesemwa leo Juni 13,2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule wakati akziungumza na waandishi wa habari kuelekea katika ziara hiyo.
Bi.Senyamule amesema kuwa Rais Samia atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato ambacho Ujenzi wake umeghariimu Sh. Billion 359 na Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje kutoka Mtumba, Veyula hadi Nala, mradi huo wenye thamani ya Shilingi bilioni 221.
“Kesho Juni 14,2025 Rais Samia atafanya ziara ya kukagua miradi katika Mkoa wetu ambapo ataambatana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mhe. Dkt. Akinwumi Adesina katika ziara hiyo”amesema Bi.Senyamule
Hata hivyo ameongeza kuwa mara baada ya kukagua maendeleo ya miradi ya Mkoa wa Dodoma Mhe.Rais Samia atahitimisha ziara yake kwa kuzungumza na wananchi wa Nala.
Aidha amesema kuwa Mkoa wa Dodoma una miradi 3,093 ya kimaendeleo iliyotekelezwa na Serikali ikiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi trilioni 10 katika kipindi kifupi cha uongozi wake.
Bi.Senyamule ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kumpokea Mhe. Rais Samia na kushiriki kikamilifu katika hafla hiyo. Tukio hili ni nafasi adhimu ya kuonyesha shukrani kwa maendeleo makubwa yanayoendelea kushuhudiwa katika Mkoa wa Dodoma, ikiwemo huduma bora za maji, afya, na elimu.
Post a Comment