Mwenyekiti wa Wasukuma Mkoa wa Mwanza na Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Mwanza Josephat Nuingwa Amesema wao kama Machifu wamepokea Maelekezo ya Chief Hangaya ambae ni Dkt Samia Suluhu Hassan kwa yale aliyowaelekeza 21/6/2025 alipotembelea Katika Kongamano la Machifu lililofanyika Wilaya ya Magu Kisesa Bujora.
Akizungumza Mweyekiti uyuu katika maeneo ya Bujora Kisesa Wilaya ya Magu Amesema Tunampongeza Mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kitambua umuhimu wao katika kundi Hilo ambalo lilikuwa limesahaulika lakini Mama uyuu amekuwa wa mfano na kutambua umuhimu wake hakika tunakila sababu ya kujivunia Rais wetu.
Nuingwa Amesema Kuhusu suala la Lamli Chonganishi tumepokea maelekezo ya Mhe, Rais na Tutayafanyia kazi nitoe wito kwa Waganga wa Tiba Asili Mkoa wa Mwanza Kupokea Maelekezo ya Mhe,Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kutojiusisha na Ramli Chonganishi alisema chief.
Post a Comment