Na Mapuli Kitina Misalaba
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kiwango cha ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania kimepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2009. Akizungumza jijini Dodoma, Dkt. Gwajima amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi mbalimbali za serikali na wadau wa maendeleo katika kukabiliana na vitendo vya ukatili.
Kwa Watoto wa Kike:
- Ukatili wa kingono umepungua kutoka asilimia 33 mwaka 2009 hadi asilimia 11 mwaka 2024.
- Ukatili wa kimwili umepungua kutoka asilimia 76 hadi asilimia 24.
- Ukatili wa kihisia umepungua kutoka asilimia 25 hadi asilimia 22.
Kwa Watoto wa Kiume:
- Ukatili wa kingono umepungua kutoka asilimia 21 hadi asilimia 5.
- Ukatili wa kimwili umepungua kutoka asilimia 74 hadi asilimia 21.
- Ukatili wa kihisia umepungua kutoka asilimia 31 hadi asilimia 16.
Dkt. Gwajima amesema kupungua kwa takwimu hizo ni ishara ya mafanikio ya mikakati ya kitaifa ya kuwalinda watoto, ikiwemo elimu ya ulinzi wa mtoto, kampeni za kitaifa dhidi ya ukatili na ushirikiano baina ya sekta mbalimbali.
Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kila mtoto analelewa katika mazingira salama, yenye upendo na heshima.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment