
Na Mapuli Kitina Misalaba
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo, Manispaa ya
Shinyanga, Victor Mkwizu, leo Juni 29, 2025, amejitokeza rasmi kuchukua fomu ya kuwania
tena nafasi ya udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mkwizu aliwasili katika
ofisi za CCM Kata ya Ngokolo kwa kutumia usafiri wa bodaboda,
kitendo kilichoashiria ukaribu wake na wananchi na maisha halisi ya watu wa
kawaida anaowawakilisha.
Fomu hiyo amekabidhiwa
na Kaimu Katibu wa CCM Kata ya Ngokolo, Jafari Juma,
mbele ya wanachama na wafuasi wa chama hicho waliomsindikiza kwa hamasa kubwa.
Akizungumza baada ya
kukabidhiwa fomu, Mkwizu amesema ameamua kutetea nafasi hiyo kwa lengo la kuendeleza jitihada za maendeleo alizozianzisha katika
kipindi cha miaka mitano aliyohudumu tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
“Nikipewa ridhaa
ya chama kuendelea kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka
huu, nitazungumza kwa kina mambo ambayo nimeyafanya kwa ajili ya wananchi wa
Ngokolo na mikakati ya kuendeleza pale tulipoishia,”
amesema Mkwizu.
Zoezi la uchukuaji fomu
kwa nafasi za udiwani linaendelea maeneo mbalimbali nchini huku wagombea
mbalimbali wakiendelea kujitokeza kutafuta ridhaa ya chama kuelekea uchaguzi
mkuu wa mwaka 2025.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment