Na Mapuli Kitina Misalaba
Kijana mzawa wa Kata ya Ngokolo, Fravian Patrick Makwaiya, leo Juni
29, 2025, amejitokeza rasmi kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania nafasi ya udiwani
katika Kata ya Ngokolo kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwaka huu.
Akipokea fomu hiyo
katika Ofisi za CCM Kata ya Ngokolo, Fravian amesema ana kiu kubwa ya kuona
maendeleo yanapatikana kwa haraka katika kata hiyo, akisisitiza kuwa akiwa
kijana mzalendo na mzawa wa eneo hilo, changamoto za maendeleo amekuwa akiishi
nazo, hivyo anauelewa wa kina kuhusu nini kinapaswa kufanywa.
“Nimezaliwa hapa,
nimelelewa hapa, na changamoto zote ninazijua kwa undani. Sasa ni muda wangu,
kama kijana mwenye damu changa na moyo wa kizalendo, kushirikiana na wananchi –
ambao ni wazazi wangu – kuhakikisha tunapambana kwa pamoja kuleta maendeleo,”
amesema Fravian.
Makwaiya ameongeza kuwa
anaamini vijana wana nafasi kubwa katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo,
hasa wanapopata nafasi ya kuongoza kwa kushirikiana na wazee na wadau wote wa
maendeleo ndani ya jamii.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment