" WATU 67 WAIHAMA CHADEMA MISSENYI WAREJEA CCM ILI KUMUUNGA MKONO EVANCE KAMENGE KWA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA MISSENYI

WATU 67 WAIHAMA CHADEMA MISSENYI WAREJEA CCM ILI KUMUUNGA MKONO EVANCE KAMENGE KWA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA MISSENYI


Na Mwandishi wetu
Missenyi 

Jumla ya watu 67 kutoka kata mbali mbali za wilaya yaMissenyi Mkoani Kagera wamejitokeza katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani  Missenyi Juni 29,2025 kwa  lengo la kumuunga mkono Evance Kamenge  aliyevuta fomu ya kugombea kiti cha ubunge Jimbo la Missenyi mnamoJuni 28,2025.

Wakizungumza baada ya kurejesha na kukabidhi kadi hizo waliokuwa wanachama wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akiwemo Remigius Daniel  aliyekuwa katibu katika kata ya Mabare kwa miaka kumi amesema amevutiwa sana na uongozi imara wa Rais Samia kwa maendeleo aliyoyafanya kwa Watanzania hususani katika wilaya ya  Missenyi huku wakieleza kuwa wanatamani jimbo hilo kuongozwa na watu mahiri na wafuatiliaji ambapo jicho lake limemuona Evance Kamenge.

Salum Masoud amesema alikuwa mnazi wa Chadema kwa miaka kumi na tano Ila kwa mabadiliko aliyoyaona hana budi kuendana na upepo anaouona kutoka kwa Kamenge kupitia maono aliyonayo.

Kwa upande wake Jackline Joseph, Ramadhan Abdallah, Apornary  Joseph,Martin Mathias,Ailin John, Mariana Thomas Elivia karoli pamoja na wengineo wamesema wamevutiwa na kauli za Evance Kamenge mgombea ubunge Jimbo la Missenyi hivyo wameamua kwendana na upepo wake wa mabadiliko wanaoamini utakwenda kuibadilisha Missenyi kwa kipindi kijacho .

wameahidi kumuunga mkono Kamenge kwani ni kijana mwenzao na ameona mbali hasa katika kubadili taswira ya kilimo na uzalishaji hivyo wanamuomba Mwenyezi Mungu ili kufanikiwa kijana huyo ambaye atawaletea maendeleo wana Missenyi na Taifa kwa ujumla

Wamesema kuwa tayari Wana imani na Rais Samia kutokana na miradi ya maendeleo aliyoifanya kwa kipindi chote kwani wameona wenye baadhi ya sekta ikiwemo Elimu, Afya, maji, Barabara vilivyo imarika na kuongeza hamasa kwao jambo lililowapa nguvu za kuungana naye.

Aidha wameahidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Kamenge ili aungane na wenzake watakaofanikiwa kupata nafasi ya ubunge na kukanyanga ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muda ukifika.

Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao waliohama CHADEMA kujiunga na CCM Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Missenyi Bakhari Mwacha  amesema kuwa amewapokea wanachama hao ambao tayari wamerejesha kadi zao na kujiunga na CCM huku akiendelea kuwasubiri watakaojitokeza ili kukamilisha idadi iliyotajwa.

Hata hivyo Katibu huyo ameongeza kuwa mchakato wa kadi za CCM unakwenda kidijitali ambapo watasajiliwa katika mfumo wa kielekroniki na taarifa hizo zitafika makao makuu na kadi zao zitatengenezwa na kuwafikia katika kata zao kupitia Katibu wa tawi husika.
















 


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post