" VIJANA WAMPONGEZA MWEKEZAJI MGODINI

VIJANA WAMPONGEZA MWEKEZAJI MGODINI


Na Mwandishi Wetu, Misalaba Media

WACHIMBAJI wadogo wa madini ya Dhahabu wilayani Bukombe Mkoani Geita wameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwawezesha eneo la uchimbaji madini hivyo kuwawezesha kujiajiri. 

Wito umetolewa Jana katika mgodi wa Dhahabu wa Saul Zephania Partiners Investment na Vijana wanaojishughulisha na uchimbaji madini mgodini hapo kutokana na fursa waliyopata ya kuweza kujiajiri kupitia shughuli hiyo.

Mkaguzi wa mgodi huo Joseph Richard alisema wanashukuru dhamira iliyooneshwa na serikali ya kuwawezesha kupata eneo la kuchimba madini pamoja na ukaguzi unaofanywa na Ofisi ya madini ya Mkoa kuwezesha uwepo wa Usalama wa kuaminika katika eneo hilo.

“Ni faraja kwetu kuona ofisi ya madini wakitutembelea na kutupatia ushauri wa kuhakikisha Usalama wetu unakuwepo” alisema Richard.

Sambamba na Pongezi hizo kwa serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Vijana hao walpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Saul Zephania Partiners Daniel Lushinge kwa kuanzisha mgodi huo na Kuwa faraja kubwa kwao.

Walisema kuwepo kwa wawekezaji wenye kujitolea kusaidia kuunga mkono juhudi za serikali ni faraja kubwa  kwa watanzania hivyo wakaomba jitihada hizo zilizoneshwa na Lushinge ziigwe na wazawa wengine.


Post a Comment

Previous Post Next Post