Na Tonny Alphonce, Misalaba Media -Mwanza
Mtandao wa Wanawake Wachakataji wa Mazao ya Uvuvi Tanzania (TAWFA) wametoa mafunzo Kwa Wanawake Wachakataji 23 juu ya matumizi ya teknolojia katika biashara kutoka mikoa ya Mwanza na Mara.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa mradi wa mtandao wa Wanawake Wachakataji Kanda ya Ziwa Kitogo Lawrence amesema wameona
Kuna umuhimu wa Wanawake waliopo katika sekta ya Uvuvi kupewa elimu ya matumizi ya mtandao ya kijamii.
"Wengi hawajui umuhimu wa kutumia mirandao ya kijamii na tukaona ni vema wabadili matumizi ya akaunti zao liwe eneo la kuzuia bidhaa zao".alisema Kitogo
Kitogo amesema katika semina hiyo ya Siku tatu Wanawake hao Wachakataji wamepewa elimu ya faida ya kusajili biashara zao na kutambulika rasimi kisheria.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Biashara na Viwanda kutoka Sido Peter Kilima amesema katika mafunzo waliyowapatia wanawake wachakataji ni pamoja na elimu ya utunzaji Bora wa bidhaa,mafunzo ya matumizi ya TEHAMA pamoja na elimu ya namna gani ya kufanya biashara ndani na nje ya nchi.
Kilima amesema ni matumaini yake Kuwa elimu hiyo waliyoitoa italeta mapinduzi makubwa katika biashara zao pamoja na kuepuka matapeli walikuwa wakiwatapeli.
"Tumewafundisha umuhimu wa mkataba na wateja,kuwachunguza pamoja na kupata taarifa zao za kina kabla ya kufanya biashara".alisema Kilima
Nao Wanawake Wachakataji Joyce Malima na Jackline Felix wameishukuru TAWFA Kwa kupataia mafunzo hayo na kuahidi kwenda kuisambaza kw Wanawake wenzao wanaofanyabiashara ya Uvuvi.
Afisa mradi wa mtandao wa Wanawake Wachakataji Kanda ya Ziwa Kitogo Lawrence akizungumza.
Post a Comment