Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Green Acres Tanzania, Bi Jacklyne Siima Rushaigo, mwenye elimu ya Shahada ya Uzamili katika Benki na Fedha (MSc), amechukua na kurejesha fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Missenyi, mkoani Kagera.
Akiwasilisha fomu yake katika ofisi ya Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoko Nyabihanga, Kyaka Missenyi, Bi Jacklyne amezungumza na waandishi wa habari na kueleza matumaini yake ya kuchaguliwa.
Amesisitiza kuwa endapo akipata rdhaa kutoka kwenye chama chake kwa nafasi ya kugombea, ataonyesha kujiamini katika uwezo wake wa kutumikia wananchi na kuwaletea maendeleo.
Bi Jacklyne ameahidi kuleta mabadiliko chanya katika jamii ya Missenyi, na kutoa kipaumbele katika masuala ya elimu, afya, na maendeleo ya kiuchumi.
Ametoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kumuunga mkono katika safari yake ya kuwakilisha Masuala ya maendeleo ya Jimbo hilo.
Bi Jacklyne ana matumaini kuwa atafanikiwa kuleta maendeleo endelevu na kuboresha maisha ya wananchi wake.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment