Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima amesema ataendelea kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), licha ya kukosolewa kila anapotoa maoni yenye mtazamo tofauti ndani ya chama hicho huku akikishauri Chama hicho kukubali ifanyike ‘REFORM’ (mabadiliko) na kubainisha kuwa haoni sababu ya CCM kuogopa wakati ina wanachama zaidi ya milioni 10.
“Mimi bado ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi na nitaendelea kuwepo. Mimi sihami, CCM nipo sana, tunabanana humu humu ndani mpaka paeleweke pakae vizuri. CCM ni chama cha kidemokrasia kama ilivyo madhumuni ya katiba yake.”
“Kushinda uchaguzi ni jambo jepesi, lakini kutawala nchi ambayo imemegukameguka kutokana na makovu na majeraha ya uchaguzi ni kazi sana.” - Askofu Josephat Gwajima
Post a Comment