" AZAM FC YAMTAMBULICHA KOCHA FLORENT IBENGE

AZAM FC YAMTAMBULICHA KOCHA FLORENT IBENGE


 

Klabu ya Azam Fc imemtambulisha aliyekuwa kocha wa Al Hilal ya Sudan, Florent Ibenge kama kocha wao mkuu klabuni hapo akichukua mikoba ya Rachid Taoussi aliyeoneshwa mlango wa kutokea baada ya kutamatika kwa msimu uliopita.

Akizungumza baada ya utambulisho huo Ibenge amesema amefurahi kupata nafasi ya kuinoa Azam FC huku akiahidi kufanya makubwa ndani ya kikosi hicho akifurahia kupata nafasi ya uwakilishi kimataifa huku akiitaja Simba na Yanga.

“Kama ligi ya Tanzania ni namba nne kwa ubora basi timu zilizopo zina ushindani mkubwa lakini anaamini amekuja kupamba ili aweze kufikia mafanikio na wao wapo kwenye nafasi ya ushindani,” alisema na kuongeza.

“Simba msimu huu imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho ni namna gani kuna timu bora lakini pia kuna Yanga ambayo imetwaa mataji yote msimu huu nahitaji ushindani mkubwa kutoka kwao nipo tayari kwa ushindani.”

Ibenge amesema anatambua ana cv kubwa lakini hiyo haitoshi kuipa mataji Azam bila kuwekeza nguvu kwenye kujenga timu bora kilichomleta Tanzania ni kuipambania timu hiyo kutwaa mataji ndani na kimataifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post