" BANDARI YA TANGA YASHAMIRI ONGEZEKO LA MELI ZA MIZIGO

BANDARI YA TANGA YASHAMIRI ONGEZEKO LA MELI ZA MIZIGO

Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian amesema maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali katika Bandari ya Tanga Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yameongeza uwezo na ufanisi wa bandari hiyo katika kuhudumia meli na shehena kubwa 

 Sambamba na hilo  meli zinazotia nanga kwa ajili ya kushusha na kupakia shehena imeongezeka kutoka  198 mwaka 2021 hadi meli 307 mwaka 2023.

Amesema hayo leo Julai 15, 2025 Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO kuelezea mafanikio ya Mkoa huo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hatahuvyo Amesema  Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania "TPA"Katika kipindi cha mwaka 2020 hadi Aprili 2025 imetekeleza mradi mkubwa wa kimkakati wa maboresho ya bandari hiyo kwa awamu mbili ambapo Jumla ya shilingi shilingi bilioni 429.1 zimetumika.

Balozi Batilda ameeleza kuwa kufuatia maboresho hayo shehena (mizigo) imeongezeka kutoka tani 888,130 mwaka 2021 hadi tani 1,191,480 zinazopakuliwa na kupakiwa kwenye makasha (TEUS) kupitia bandari hiyo kutoka 7,036 hadi makasha 7,817 ambapo pia muda wa kuhudumia meli umepungua kutoka siku 5 hadi siku 2.


Katika hatua nyingine Mhe. Balozi Batilda Burian amesema kuwa Mkoa wa Tanga umepokea shilingi trilioni 1.118 kwajili ya ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV Tanga ili kusaidia wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post