" Kassim Majaliwa Ataja sababu ya Kustaafu Kugombea Ubunge Jimbo la Ruangwa

Kassim Majaliwa Ataja sababu ya Kustaafu Kugombea Ubunge Jimbo la Ruangwa

 

Taarifa rasmi kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari nchini Tanzania zinaeleza kwamba Waziri mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza rasmi kustaafu kugombea ubunge kwenye jimbo la Ruangwa.

Chanzo cha taarifa hii kimeeleza wazi kwamba Kassim Majaliwa amefikia maamuzi ya kustaafu kugombea katika jimbo hilo mara baada ya kukitumikia jimbo hilo kwa jumla ya miaka 15 mpaka sasa.

Inaelezwa kwamba Kassim Majaliwa alikuwa na mpango wa kugombea tena ubunge kwa awamu hii na tayari alikuwa anafanya mipango ya kutengeneza mchakato ya kuchukua fomu tena kwa lengo ya kuingia kwenye mchakato wa kura za ndani kutoka kwa wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi yaani CCM.

Mambo yamebadilika gafla kwani mpaka sasa inaelezwa kwamba Kassim Majaliwa amebadilisha mawazo ya kuendelea kugombea kwenye jimbo hilo na ameomba kupumzika kwa maana ya kutoa nafasi kwa wagombea wengine ambao wametia nia kwenye jimbo hilo.

Siku chache zilizopita Kassim Majaliwa alikutana na wazee wa Ruangwa ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ambapo alizungumza nao mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na mpango wake wa kubadili mawazo ya kuendelea kugombea tena nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Wazee wa Ruangwa wamebariki maombi ya Kassim Majaliwa na sasa ni wazi kwamba amejiengua kwenye mchakato huo wa uchaguzi licha ya kwamba wananchi wa Ruangwa walikuwa wanategemea kuona jimbo lao linakuwa chini yake kuelekea katika miaka mitano ijayo.

CCM watalazimika kumsimamisha mgombea mpya ambaye atakuwa na sifa sawa kama ilivyokua kwa Kassim Majaliwa ambaye kwa 15 aliyodumu madarakani tayari ameacha alama bora katika jimbo hilo kubwa mkoani Lindi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post