" NAOMBA TENA RIDHAA YA KUTETEA KITI CHA UBUNGE HAPA NYUMBANI ” – MHE. KATAMBI BAADA YA KUREJESHA FOMU KWA UJASIRI NA MATUMAINI

NAOMBA TENA RIDHAA YA KUTETEA KITI CHA UBUNGE HAPA NYUMBANI ” – MHE. KATAMBI BAADA YA KUREJESHA FOMU KWA UJASIRI NA MATUMAINI



Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Paschal Patrobas Katambi, leo Julai 2, 2025, amerejesha rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania tena Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Katambi ameushukuru uongozi wa chama hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na wananchi wa Shinyanga kwa ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi cha miaka mitano ya utumishi wake.

"Nimerudisha fomu hii leo lakini nipende kutoa shukrani zangu kwa viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na wananchi wote kwa ushirikiano mkubwa walionionyesha kwa miaka mitano ambayo nimekuwa Mbunge wa Jimbo hili lakini nimerudi kuomba tena ridhaa ya kutetea kiti cha Ubunge nikiwa na imani, nguvu na ari mpya ya kuendelea kulitumikia Jimbo letu la Shinyanga Mjini" -  amesema Mhe. Katambi.

Aidha, Mhe. Katambi amesisitiza kuwa mafanikio yote yaliyopatikani na utekelezaji wa miradi ya maendeleo yamechochewa na ushirikiano mkubwa ambao umejengwa na mshikamano wa wananchi, viongozi wa chama,watumishi mbalimbali wa taasisi za Serikali na binafsi.

Katambi ameahidi kuendeleza kasi ya maendeleo katika Jimbo hilo endapo atapata tena nafasi ya kuwa Mbunge  huku akiwashukuru pia waandishi wa habari kwa kuelimisha na kufikisha taarifa sahihi kwa jamii.




Post a Comment

Previous Post Next Post