" NYASANI AREJESHA FOMU YA UDIWANI KATA YA NGOKOLO

NYASANI AREJESHA FOMU YA UDIWANI KATA YA NGOKOLO

Na Mapuli Kitina Misalaba

Afisa Ununuzi na Ugavi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga, Alfred Alex Nyasani, maarufu kama Nyasani, leo Julai 2, 2025, ameonyesha dhamira ya kuwatumikia wananchi kwa sura mpya baada ya kuchukua na kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani wa Kata ya Ngokolo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nyasani amechukua fomu hiyo asubuhi katika ofisi za CCM kata ya Ngokolo, na kurejesha rasmi siku ya leo, jambo lililowavutia watu wengi  kushuhudia msanii na mtumishi wa umma akifanya maamuzi ya kisiasa kwa ajili ya maendeleo ya jamii yake.

Mbali na taaluma yake ya ununuzi na ugavi, Nyasani ni msanii wa Bongo Fleva anayezidi kujizolea mashabiki kutokana na kazi zake zenye ubora na ujumbe mzito. Hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya uitwao “SAWA”, akiwa amemshirikisha mkongwe wa muziki Mr. Blue, wimbo ambao unaendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa ya muziki mtandaoni.

Kwa sasa, macho yote yameelekezwa Kata ya Ngokolo, ambako jina la Nyasani linaanza kutikisa si kwa muziki tu, bali pia kwa matumaini ya mabadiliko ndani ya uongozi wa mitaa.
Afisa Ununuzi na Ugavi wa TANROADS Shinyanga ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Alfred Alex Nyasani "Nyasani", awali akipokea fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Udiwani Kata ya Ngokolo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mapema leo Julai 2, 2025.
Afisa Ununuzi na Ugavi wa TANROADS Shinyanga ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Alfred Alex Nyasani.

Post a Comment

Previous Post Next Post